RAMEPRO YAPAZA SAUTI, YATAKA HATUA ZA HARAKA KUTATUA KERO YA MAJI DAR ES SALAAM
.jpeg)
Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa Serikali na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji inayowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.
Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Tandale, Manzese Mtogole, Tiptop, Mabibo na Magomeni Kagera, ambapo wananchi wanakabiliwa na usumbufu mkubwa wa upatikanaji wa maji kwa matumizi ya kila siku.
Kwa mujibu wa TRAMEPRO, baadhi ya wananchi wanalazimika kununua dumu la maji la lita 20 kwa Shilingi 600 hadi 1,000, hali inayoongeza gharama za maisha, hususan kwa familia zenye kipato cha chini.
Kupitia taarifa iliyotolewa Novemba 5, 2026, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Boniventura F. Mwalongo, ameitaka Serikali kuweka mpango wa dharura wa usambazaji wa maji safi na salama, kusimamia bei za maji pamoja na kutoa taarifa sahihi kuhusu sababu za changamoto hiyo.
TRAMEPRO imesisitiza kuwa maji ni haki ya msingi na nguzo muhimu ya afya ya jamii, huku ikiitaka Serikali kutoa majibu ya vitendo kwa kuwa wananchi wanahitaji maji sasa, si ahadi za kesho.
No comments: