NMB yaja na zawadi za Sh milioni 600 kwa wateja.

Benki ya NMB imezindua kampeni ya Bonge la Mpango ‘Weka na Ushinde’, ikitenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 600 kwa wateja wanaoweka akiba. Kampeni hiyo iliyoanza Novemba Mosi na kuendelea hadi Januari 31, 2027, inahusisha zawadi za fedha taslimu, pikipiki na magari matatu. 

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam Novemba 3, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema wateja 130 watapata Sh 100,000 kila mmoja kupitia droo 13 za kila wiki, huku wengine 30 wakipata Sh 500,000 kila mmoja kupitia droo za kila mwezi. Zawadi kuu zitakuwa Toyota Land Cruiser la utalii na Ford Ranger mbili. 

Mponzi alisema kampeni hiyo pia inahusisha vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) katika mikoa ya Mtwara na Lindi, ambapo pikipiki zaidi ya 20 zimetengwa kwaajili ya vyama vitakavyo pitisha malipo ya zao la korosho kupitia NMB katika msimu wa 2026/2027. 

Mkuu wa Matawi na Mauzo wa NMB, Donatus Richard, aliwataka Watanzania kufungua akaunti na kuweka akiba, akisema huduma za kidijitali za NMB Mkononi zinawawezesha wateja kufanya miamala na kupata huduma mbalimbali za kibenki, ikiwemo mikopo ya hadi Sh milioni tano bila dhamana.



 

No comments: