JUMUIYA YA MARIDHIANO NA AMANI YAMFARIJI RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salumu, akiongoza ujumbe wa jumuiya hiyo kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 11 Septemba 2026, kufuatia kufiwa na mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar, tarehe 7 Septemba 2026.

Kwa upande wake, Balozi wa Amani nchini Tanzania, Mess Chengula, alitoa salamu za pole kwa Mhe. Rais, familia na Watanzania kwa ujumla, akiwasihi kuwa na subira na mshikamano katika kipindi hiki cha majonzi.















No comments: