FUVU LA MKWAWA, MAKABURI YA MACHIFU, VYAVUTA WAGENI KALENGA
Mkoa wa Iringa unaendelea kujivunia urithi muhimu wa kihistoria kupitia Makumbusho ya Mtwa Mkwawa yaliyopo katika kijiji cha Kalenga, Wilaya ya Iringa Vijijini, takribani kilomita 12 kutoka Manispaa ya Iringa.
Makumbusho hiyo inayosimamiwa na Makumbusho ya Taifa la Tanzania, imeendelea kuwa kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi wanaofika kujifunza historia ya jamii ya Wahehe na kumuenzi Chifu wa Wahehe, Mkwawa ambaye alijulikana kwa msimamo wake wa kupinga utawala wa kikoloni.
Mhifadhi wa Mambo ya Kale katika Makumbusho ya Mtwa Mkwawa, Zuhura Mohamed, amesema eneo hilo lina umuhimu mkubwa katika kuhifadhi historia, utamaduni na kumbukumbu za jamii ya Wahehe, huku likitoa fursa kwa vizazi vya sasa na vijavyo kujifunza historia kwa vitendo.
Miongoni mwa vivutio vikuu vinavyowavutia wageni katika eneo hilo ni fuvu linalotambuliwa kuwa la Chifu Mkwawa, mmoja wa viongozi mashuhuri wa Wahehe katika historia ya Tanzania.
Eneo la Makumbusho ya Mtwa Mkwawa pia linahifadhi makaburi ya baadhi ya machifu pamoja na majengo ya kihistoria yanayotoa picha ya maisha ya jamii na mabadiliko yaliyotokea katika eneo hilo wakati wa utawala wa kikoloni.
.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

No comments: