Airtel Tanzania yaimarisha ushirikiano wa kimkakati kupitia Airtel Business Monthly Mug Tournament
Arusha, 4 Agosti 2026 – Airtel Tanzania imeendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kimkakati na wateja kupitia mashindano ya Airtel Business Monthly Mug Tournament yaliyofanyika katika Klabu ya Gymkhana jijini Arusha, Tanzania.
Mashindano hayo yaliwaleta pamoja viongozi wa biashara, wateja, na wadau mbalimbali, yakitoa fursa ya kujenga mahusiano yenye tija, kubadilishana mawazo, na kutambua fursa mpya za ukuaji wa biashara nje ya mazingira ya kawaida ya kikazi sambamba na kutambua na kuunga mkono mchezo wa Gofu nchini.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Airtel Business, Joseph Vipond, alisema Airtel inaamini ushirikiano imara hujengwa kupitia mawasiliano ya karibu na ushiriki endelevu, huku michezo ikitoa jukwaa bora la kuimarisha mahusiano hayo.
Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano kwa Umma wa Airtel Tanzania, Sarah Nassor, alisema mashindano hayo yanaonyesha dhamira ya kampuni ya kujenga uhusiano wa kudumu na wadau kwa kuwashirikisha katika masuala yanayochochea mawasiliano, uaminifu, na ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
Moja wa watumiaji wa huduma za Airtel Bw. Hiten Nathwani, ameipongeza kampuni ya Airtel kwa kuendelea kuboresha huduma zake sambamba na kuwasihi wachezaji Gofu hao kutumia huduma za Airtel.
Kupitia Airtel Business Monthly Mug Tournament, Airtel Tanzania inaendelea kuonyesha kuwa ushirikiano wenye tija hujengwa zaidi ya mahusiano ya biashara kwa kuunganisha watu toka sehemu mbalimbali na kuunganisha jamii ili kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi jumuishi wa kidijitali nchini.

.jpeg)
.jpeg)

No comments: