WAANDISHI WA HABARI WANANUFAIKA NA HUDUMA ZA JAB SABASABA
Dar
es Salaam. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea
kutoa huduma mbalimbali kwa waandishi wa habari, wadau wa sekta ya
habari na wananchi kupitia banda lake lililopo katika Kijiji cha Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Maonesho ya 50 ya
Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Huduma
zinazotolewa ni pamoja na ugawaji wa vitambulisho vya ithibati kwa
waandishi wa habari waliokidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za
Habari, Sura ya 229, usajili wa waandishi wa habari, marekebisho ya
taarifa za usajili pamoja na utoaji wa elimu kuhusu majukumu na huduma
mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo.
JAB imesema ushiriki wake
katika maonesho hayo unalenga kusogeza huduma karibu na wananchi na
wadau wa sekta ya habari, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma pamoja
na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa ithibati na usajili wa waandishi wa
habari nchini.
Bodi hiyo imewahimiza waandishi wa habari na
wadau wengine kutumia fursa ya maonesho hayo kupata huduma kwa haraka na
kwa ukaribu, huku ikieleza kuwa huduma hizo zinaendelea kutolewa pia
katika Makao Makuu ya JAB.
Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya
Biashara ya Dar es Salaam yanaendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius
Nyerere, Barabara ya Kilwa, yakihusisha taasisi mbalimbali za umma na
binafsi zinazowasilisha huduma na bidhaa zao kwa wananchi.

















No comments: