Dkt. Josephine Rogate Kimaro Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wanne aliowateua hivikaribuni, wakiwemo majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amewaapisha viongozi hao leo, tarehe 24 Julai 2026, katika hafla iliyofanyika IkuluZanzibar.
Viongozi waliokula kiapo ni:
1. Dkt. Mahadhi Juma Maalim Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.
2. Mhe. Valentina Andrew Katema Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
3. Mhe. Khamis Ali Simai Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
4. Dkt. Josephine Rogate Kimaro. Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla; Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zuberi AliMaulid; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndg. Mansoura Mossi Kassim; pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini na wageni wengine waalikwa..jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

No comments: