Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Yaweka Mkazo Usimamizi Bora wa Miradi

 

Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar Mhandisi Ali Said Bakar akizungumza katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya 16 ya Siku ya Mabaharia Duniani mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar Mhandisi Ali Said Bakar akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia mara baada ya kufungua wa Maadhimisho ya 16 ya Siku ya Mabaharia Duniani mkoani Kigoma.

Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya Umwagiliaji imewakutanisha Menejimenti, Wahandisi wa Mikoa, Wakandarasi pamoja na Washauri Elekezi katika kikao kazi maalumu chenye lengo la kujadili namna ya kuboresha usimamizi wa miradi ya umwagiliaji ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ubora unaohitajika na kukamilika kwa wakati.

Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mdolwa, na kuwahusisha viongozi mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini. Lengo kuu lilikuwa kujadili utaratibu mpya wa usimamizi wa miradi ya umwagiliaji pamoja na kuweka mikakati itakayoongeza ufanisi katika utekelezaji wake.

Washiriki walijadili kwa kina hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi inayoendelea nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, huku ikizingatia viwango vya ubora vilivyowekwa.

Aidha, kikao hicho kilisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wakandarasi, washauri elekezi na wataalamu wa Tume katika kusimamia, kulinda na kutunza mali za umma zinazotumika katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miundombinu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Leopold Runji, alieleza kuwa maandalizi ya taarifa sahihi na ushirikiano wa karibu kati ya wadau wote ni muhimu katika kufanikisha malengo ya Serikali kwenye sekta ya umwagiliaji.

“Ni muhimu kufanya kazi kwa ukaribu na kwa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya Serikali katika sekta ya umwagiliaji,” alisema Runji.

Kwa upande wao, Washauri Elekezi walioshiriki kikao hicho waliipongeza Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kuwaamini na kuwapa jukumu la kusimamia miradi mbalimbali. Pia walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana, kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa mafanikio makubwa.Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Yaweka Mkazo Usimamizi Bora wa Miradi
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Yaweka Mkazo Usimamizi Bora wa Miradi




Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya 16 ya Siku Mabaharia Duniani.

No comments: