Senegal dhidi ya Iraq Mchezo wa Maamuzi Mashindano Dunia 2026
SENEGAL na Iraq wanakutana katika mechi ya mwisho ya Kundi I huku timu zote zikiwa na alama sifuri baada ya mechi mbili. Ushindi pekee ndio unaweza kuweka matumaini ya kufuzu kwa hatua ya 32 Bora, kwani timu nane kati ya kumi na mbili zinazomalia nafasi ya tatu katika makundi zitaingia hatua ya mtoano. Senegal wako katika nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao -3, huku Iraq wakiwa wa nne na -6.
Senegal wamepoteza mechi zote mbili dhidi ya Ufaransa (3-1) na Norway (3-2), lakini wamefanikiwa kufunga mabao matatu, mawili yakifungwa ya Ismaila Sarr. Iraq wamefungwa mabao saba katika mechi mbili, wakifunga bao moja tu kupitia Aymen Hussein dhidi ya Norway. Ushindi wa Iraq dhidi ya Uhispania katika mechi ya kirafiki ulitoa matumaini kidogo, lakini michuano ya Dunia imefunua udhaifu wao.
Senegal wana safu ya mashambulizi yenye nguvu ikiwa na Sadio Mane, Ismaila Sarr, na Nicolas Jackson. Mane ndiye mfungaji bora wa Senegal katika historia akiwa na mabao 55 katika mechi 127, huku Sarr akiwa ameshafunga mabao mawili katika michuano hii .
Iraq wanategemea kipa Jalal Hassan na mshambuliaji Aymen Hussein. Makabiliano muhimu ni pamoja na winga wa Senegal Ismaila Sarr dhidi ya beki wa kushoto Merchas Doski, pamoja na kiungo Idrissa Gueye dhidi ya Amir Al-Ammari.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Senegal wanatarajiwa kushinda mechi hii kwa urahisi kutokana na ubora wa wachezaji wanaocheza Ulaya, huku wachezaji wengi wa Iraq wakitokea ligi za ndani. Senegal walifunga mabao 16 katika mechi sita za kufuzu, wakifunga mabao manne katika mechi mbili za mashindano ya Dunia. Iraq wamefungwa mabao saba katika mechi mbili, na inaonekana ni vigumu kwao kuzuia mashambulizi ya Senegal. Senegal wana nafasi kubwa ya kushinda na kufunga zaidi ya mabao mawili .
Mechi hii ni fursa kwa Senegal kurejesha heshima yao baada ya kuanza vibaya, na pia ni nafasi kwa Iraq kufanya historia kwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye mashindano haya tangu 1986 . Hata hivyo, tofauti ya ubora kati ya timu hizi mbili inatarajiwa kuonekana uwanjani, na Senegal ndio wanaotarajiwa kuibuka na ushindi.

No comments: