Atletico, PSG Wapewa Nafasi Kubwa Kutinga Nusu Fainal UCL

 

BAADA ya kusubiri kwa wiki moja, leo usiku mashabiki wa soka duniani watashuhudia michezo ya kisasi ya robo fainali ya UEFA Champions League, ambapo mechi mbili kali zitapigwa kwa wakati mmoja kuanzia saa 10:00 usiku.

Huko Hispania, Atletico Madrid watakuwa nyumbani kwenye dimba la Wanda Metropolitano kuwakaribisha Barcelona wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Spotify Camp Nou. Barcelona watalazimika kupambana kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kusawazisha matokeo hayo.

Pamoja na ubora wa safu ya ushambuliaji ya Barcelona inayowaongozwa na Robert Lewandowski, Marcus Rashford na Lamine Yamal, timu hiyo inakabiliwa na changamoto ya majeruhi na wachezaji waliokosekana, hali inayoweza kuathiri mipango yao ya kutafuta ushindi.

Kwa upande wa Atletico, licha ya kukumbwa na majeruhi ya baadhi ya nyota wao, wanatarajiwa kucheza kwa tahadhari wakitumia mbinu za kujilinda na kushambulia kwa kasi kupitia Antoine Griezmann na Julián Álvarez, huku wakiaminiwa kuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Katika mchezo mwingine, Liverpool watakuwa dimbani Anfield kuwakaribisha mabingwa watetezi Paris Saint-Germain baada ya kufungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza. Liverpool wanahitaji ushindi mkubwa ili kurejea kwenye ushindani wa kufuzu hatua inayofuata.

Hata hivyo, hali ya kikosi cha Liverpool pamoja na majeruhi ya wachezaji muhimu inaweza kuwa kikwazo, huku PSG wakionekana kuwa na kikosi imara chenye nyota kama Ousmane Dembélé na Khvicha Kvaratskhelia wenye uwezo wa kuamua matokeo wakati wowote.

Kwa ujumla, Atletico Madrid na PSG wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali, huku mechi zote zikitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na matokeo yasiyotabirika.

No comments: