Turaco Collection Yashiriki Maonyesho Makubwa Ya Utalii (ITB-Berlin-2025) Nchini Ujerumani
Turaco Collection yashiriki Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama ITB -Berlin yaliyofanyika nchini Ujerumani tarehe 4-6 March 2025.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata akiziwakilisha hotel zao katika maonesho hayo ya ITB- Berlin anasema kwamba, maonesho hayo ni eneo jema kabisa la kujitangaza kubadilishana uzoefu hasa katika dunia ambayo walaji (watumiaji wa huduma) wamekuwa wakibadilika kutokana na mazingira yanayotokea duniani.
Turaco Collection kwa upande wa Dar es Salaam wana Element By Westin Marriott na Delta By Marriott na kwa upande wa utalii wa kaskazini pamoja na bidhaa mbalimbali za utalii pia wana; Turaco Ngorongoro Valley Lodge Tribute portfolio under Marriott International na Turaco Manyara View Lodge Tribute portfolio under Marriott International na kwa Zanzibar wana Turaco Nungwi Beach Reasort Tribute portfolio under Marriott International na Turaco Spice Tree Stone Town Tribute portfolio under Marriott International na Beyt Aly Salaam-By Turaco.
No comments: