PPPC YATOA MAFUNZO YA UWEKEZAJI KUPITIA UBIA KWA MADIWANI WA ILEMELA

KITUO Cha Ubia kati Serikali na Sekta binafsi(PPPC) kimetoa mafunzo namna ya uwekezaji kupitia Ubia kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza ambao wameambatana na Menejimenti ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Uongozi wa CCM wa Wilaya hiyo.

Akizungumza leo Januari 8, 2025 katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za PPPC Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, amesema serikali imekuwa ikipata hasara kutokana na ufanisi mdogo wa uendeshaji wa baadhi ya miradi, hivyo kuna umuhimu wa kukaribisha sekta binafsi ili kuleta tija na ufanisi.

Amesema katika ufafanuzi wa kuhusu masuala ya ubia amesema barabara zitakazojengwa na sekta binafsi zitakuwa ni za kulipia, lakini kutakuwa na barabara mbadala ili mtu asilazimike kukosa barabara ya kupita.

“Hakuna atayelazimishwa kupita barabara ya kulipia kwa sababu kutakua na isiyo ya kulipia, kama hauna haraka sana utapita kwenye barabara isiyo ya kulipia na kwamba hii itasaidia kupunguza msongomano barabarani” amesema Kafulila.

Kwa upande wake Mbunge wa Ilemela, Dkt. Angeline Mabula, amesema Manispaa ya Ilemela inakwenda kuwa Manispaa bora katika uwekezaji kufutia elimu waliyoipata katika kituo cha PPPC, kwa kuwa ina fursa kutokana na sehemu kuwa ya eneo lake kuwa pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Naye, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga, amesema elimu waliyoipata itasaidia katika vikao vyao vya madiwani kupitisha miradi ya ubia ili kuchochea maendeleo ya Ilemela.

Hadi sasa hapa nchini Manispaa zinazotekeleza baadhi ya miradi yake kupitia Ubia kati ya Sekta ya umma na Sekta Binafsi-PPP, ni Manispaa ya Ubungo inayotekeleza mradi wa Kituo cha Pamoja cha Kibiashara eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, na Manispaa ya Ilala inayotekeleza mradi wa DDC Kariakoo.










No comments: