NSSF YAIPONGEZA ZANZIBAR HEROES KWA USHINDI WA KOMBE LA MAPINDUZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, amepokea kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama pongezi kwa ushindi wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes). Timu hiyo ilishinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burkina Faso katika mchezo wa fainali wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika tarehe 13 Januari 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa Mhe. Rais na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Bi. Lulu Mengele, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba. Kulia kwa Mhe. Rais ni Mhe. Mama Mariam Mwinyi, na kushoto kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, pamoja na Mhasibu wa NSSF, Bi. Sirinael Mwakyusa.

NSSF ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Kombe la Mapinduzi 2025.




No comments: