NIDA YARUHUSU NDUGU JAMAA KUCHUKULIANA KITAMBULISHO CHA TAIFA, YAWATOA HOFU WANANCHI KUFUNGIWA NAMBA

 

 Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 21,2025. kuhusiana na masuala mbalimbali ya Vitambulisho vya Taifa.

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeruhusu kuchukuliana kitambulisho cha Taifa na  mtu mwingine ambaye mhusika atamwomba amchukulie.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 21,2025. Amesema kuwa baadhi ya wananchi ambao wakati wanajisajili walikuwa mahali au eneo tofauti na wanapoishi sasa wataruhusiwa kuwatumia ndugu zao ujumbe mfupi pamoja na namba zao za NIDA ambao wametumiwa kwenye simu zao na ndugu watawachukulia vitambulisho vyao katika kata, Kijiji, Wilaya ambako walijiandikishia.

"Tumeruhusu mtu huyo kuchukuliwa Kitambulisho chake na ndugu au jamaa yake. Sharti pekee tuliloliweka ni huyo mtu anayekwenda kumchukulia Kitambulisho chake aende akiwa na ujumbe mfupi 'meseji' tuliyoituma kwa huyo mwenye Kitambulisho na namba ya NIDA kwa anayechukuliwa na anayemchukuliwa mwenzake." Amesema Kaji

Pia amewaasa wananchi kutokuwa na kisingizo chochote kuhusu mtu kutokuwepo katika eneo lake la awali ambako ndiko Kitambulisho chake kilikuwa kimepelekwa.

Ameeleza kuwa anaweza akamtuma mtu kwenda kumchukulia katika ofisi ya Wilava va NIDA alikokuwa wakati anajisajili.

Licha ya hayo Kaji amewatoa hofu wananchi ya kufungiwa Namba zao za Utambulisho wa Taifa, badala yake wajitokeze kwenda kuchukua vitambulisho vyao mara wapatapo ujumbe mfupi wa simu.

"Wananchi watekeleze jukumu lao la kwenda kuchukua Vitambulisho vyao kama inavyoelekezwa katika ujumbe wa sms wanazopokea." Amesema Kaji
Akizungumzia wananchi ambaohawajapokea ujumbe mfupi kaji naomba wananchi ambao hawajapokea ujumbe mfupi wa simu kwa sasa

wasifike katika Ofisi zetu za NIDA kufuata vitambulisho, wasubiri wamalize kwanza zoezi hili maalum baadae wataendelea kutoa vitambulisho kwa watu wengine.

Kaji pia ametoa ufafanuzi kuhusiana na suala la baadhi ya vitambulisho kufutika maandishi au sura, amesema na Waziri wa Mambo ya Ndani alishalitolea maelekezo kwao ya kuchapisha vitambulisho upya kwa wale ambao vitambulisho vyao vimefutika bila malipo yeyote.

"Bahati nzuri tulikuwa tumeshaanza kufanya hivyo hata kabla ya maelekezo hayo ya Waziri. Tuliwatangazia wananchi wote wenye vitambulisho vyenye changamoto hiyo kuvirudisha katika ofisi za NIDA za Wilaya au katika ofisi za Kata, vijiji, na Mitaa vilikokuwa vimepelekwa kabla ya kuanza zoezi hili la kukusanya vitambulisho na kutuma SMS.

Ameeleza kuwa jumla Vitambulisho 31,000 vilivyokuwa vimefutika vilipokelewa, vitambulisho hivyo tayari vimechapishwa upya na vinaendelea kugawiwa.

Aidha, NIDA inaendelea kukusanya Vitambulisho vyote vyenye changamoto kwa ajili ya kuvichapisha Upya.

Aidha ametoa wito kwa mwananchi yeyote ambaye Kitambulisho chake kitakuwa na changamoto ya kufutika tafadhali akirejeshe katika ofisi ya NIDA ya Wilaya anayoishi lengo la kuvichapisha upya na kugawiwa kwa wahusika bure bila malipo yeyote.

No comments: