WAZIRI NAPE AONGOZA MAMIA YA WANANCHI JIJI LA MWANZA KUMUOMBEA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN


*Ni katika tamasha maalumu la kumuombea Rais mungu ampe hekima, busara

*Asema huu sio wakati wa kulalamika, kila mtu atamke baraka kwa ajili ya nchi

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Mwanza

TAMASHA maalumu la kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa kwa ujumla limefanyika katika Jiji la Mwanza huku Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kumuombea Rais ili Mwenyezi Mungu ampe hekima na busara katika kuliongoza Taifa letu.

Akizungumza kwenye tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Msama Promotion Nape ambaye amemuwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana aliyekuwa mgeni rasmi, amesema Kinana ameshindwa kufika kwenye tamasha hilo kwasababu amepata dharura, hivyo amemwakilisha.

“Nilisema nifike nitoe salamu zake yeye anawapenda sana na anashukuruni kwa kujitokeza kwa wingi na anamshukuru Msama Promotion kwa kuandaa tamasha hili lakini ninazo salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan.

“Wakati nakuja nimemwambia Mama nakwenda kwa Wana Mwanza wanataka kukuombea una maneno gani?Akasema la kwanza anatoa pole kwa Kanda ya Zima kwa ajali ya ndege iliyotokea , anawaomba muwe wapole Mwenyezi Mungu anaipenda nchi yetu tutavuka salama.Pili anawapenda sana alikuwa huku mlijotokeza kwa upendo mkapokea na mnaendelea kuchapa kazi , analeta salamu zake za upendo mkubwa kwenu,”amesema Nape.

Ameongeza jambo la tatu amesema Rais Samia amemwambia kuwa kuongoza nchi sio kazi rasihi, kuongoza watu wote inahitaji rehema ya Mungu, hivyo nenda kaawambie wana Mwanza waniombee neema ya Mungu juu yangu niongoze kwa haki.

“Na mimi naleta moyo wake juu yake muombeeni Rais kuongoza sio kazi rahisi , anahitaji hekima, anahitaji busara, anahitaji maarifa lakini anahitaji afya njema. Ndani ya moyo wake kumejaa haki na angetamani haki hiyo ifike kila kona ya nchi yetu.

“Anaomba mumuombee Mungu akinyoosha mkono wake juu yake haki katika nchi yetu itasimama na haki hiyo itainua nchi yetu na ninyi mnajua wana Mwanza na watumishi wa Mungu mnajua kuna nguvu kubwa sana katika kukiri kwetu kama kuna neema Mungu alimpa mwanadamu kuliko viumbe vyote ni nguvu ya kukiri.

“Mungu anasema uzima na mauti viko katika ulimi wetu tunasema nini juu ya nchi yetu , leo wana Mwanza hebu tuseme baraka juu ya nchi yetu , tuseme baraka juu ya maisha yetu , tuseme baraka juu ya Rais , tuseme baraka juu ya wasaidizi wake. Tuondoke kwenye kulalamika tutumie ulimi wetu kutamka mema juu ya nchi yetu yale tutakayotamka itakuwa roho itaishi na nchi itabarikiwa,”amesema Nape.

Akiendelea kuzungumza wakati wa maombi hayo Nape alisema kwamba kila mmoja asimame kwa miguu aseme Mungu ibariki Tanzania , Mungu mbariki Rais , ninabaraki wanaomsaidia , nina bariki uchumi wetu, nina bariki vyombo vya kutoa haki.

“Kwa hakika ndimi zetu zitabadilisha , watu wa Mungu tuondoke kwenye kulalamika, kila neno unalolisema ni roho ukisema baya linakuwa baya kama Mungu aliweka uwezo ndani ya adamu inawezekana tukatamka baraka kwa ajili ya nchi yetu, kila moja tamka baraka kwa ajili ya Tanzania , wakati wa kunung’unika umeisha.

“Tutamke Baraka na hakika itakuwa na huo ndio ujumbe ambao nimeuleta jioni ya leo , kila mmoja tamka baraka kwa maisha yako , uchumi wako , kwa watoto wako, tamka baraka , na kwa hakika itakuwa.Nyoosha mkono sema Mungu ninatamka baraka kwa nchi yangu , aridhi niliyoikanyaga naibariki, shughuli ninazofanya ninazabariki.

“Umeniahidi niweke mkono utanibariki , bariki watoto wa nchi hii , bariki wazazi wa nchi hii , bariki viongozi wa nchi hii , shusha neema yako kwa Rais wetu, mpe busara na hekima, bariki wanaomsaidia ,ibariki nchi yetu , bariki mazo yetu , bariki shughuli zetu , bariki huduma zetu , tunakuamini Mungu katika jina la yesu kristo,”amesema Waziri Nape wakati wa tamasha hilo.


Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akishiriki katika tukio la Maaskofu kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati mmoja wa maaskofu hao kutoka makanisa ya Mwanza Askofu Charles Sekelwa akifanya maombi wakati wa Tamasha hilo la lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.



Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akizungumza na kutoa salamu zake mara baada ya kufanyika kwa maombi ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.



Mwimbaji Akilimali Tumaini kutoka nchini Kenya akitumbuiza katika tamasha hilo.



Mwimbaji Joshua Ngoma kutoka nchini Rwanda akitumbuiza katika tamasha la Kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumapili Novemba 6,2022.





Waimbaji wa kwaya ya Zablon Singers wakitumbuiza Katika Tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewakilishwa na Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye





Mwambaji nyota wa muziki wa Injili nchini Tanzania Rose Muhando akitumbuiza mbele ya mamia ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokez kwenye tamasha hilo la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan pamoja na Taifa kwa ujumla

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ambwene Mwasongwe akitumbuiza Katika Tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye alishwa na Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye.

Maombie yakiendelea




Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama iliyoandaa tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa dini waliofika kushiriki tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumapili Novemba 6,2022


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akipokelewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama iliyoandaa tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati alipomwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumapili Novemba 6,2022




Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ili kushiriki katika tamasha hilo kama mgeni rasmi.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akiongozwa kuelekea jukwaani kushiriki tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akisalimiana na mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhando kabla ya kuanza kwa maombi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza


No comments: