Spika Dk Tulia Aguswa na Jitihada za Wanawake Benki ya NBC kuwanoa wenzao kiuchumi, atoa angalizo

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya NBC kupitia Chama cha wanawake Wafanyakazi wa NBC (Women Network Forum) katika kuendesha mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwakomboa wanawake dhidi ya changamoto za kiuchumi.


Kwa mujibu wa Dk Tulia jitihada mbalimbali zinazofanywa ili kuwakomboa wanawake kijamii zinaweza zisifanikiwe vema iwapo kipaumbele hakitawekwa katika kuwapatia mafunzo yanayolenga kuwajenga kiuchumi.

Spika Dk. Tulia alitoa rai hiyo jijini Dodoma leo wakati akifungua semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofahamika kama “Pamoja na NBC Bank” .

Kwa mujibu wa Dk. Tulia, kupitia mafunzo hayo wanawake wataweza kubadili fikra zao kuhusu vipaumbele vyao pindi wanapofanya maamuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa kuwa licha ya jitihada mbalimbali za wanawake nchini katika kujiongezea kipato bado changamoto imebaki kwenye namna ambavyo wanatumia kipato chao.

“Nitolee mfano mdogo tu kwenye VICOBA, ni kweli wananawake tunafanikiwa kujiongezea kipato lakini sehemu kubwa ya kipato hiki mara nyingi imekuwa ikielekezwa kwenye matumizi yasiyo ya kipaumbele ikiwemo manunuzi ya mavazi mengi zikiwemo sare nyingi tunazoshona au kununua kwa ajili ya kila tukio tunalolifanya kina mama. Ndio maana nawapongeza Benki ya NBC kwasababu kupitia wabunge hawa elimu hii itawafikia wanawake kote nchini.’’ Alisema.

Alisema mbali na kuwasaidia wabunge wanawake ambao pia baadhi yao wamekuwa na udhaifu kwenye nidhamu ya matumizi ya fedha zao, semina hiyo pia itasaidia kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya kiuchumi wabunge hao hususani pale wanaposhiriki kwenye mijadala ya kibunge inayolenga kuishauri serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi yanayowahusu wanawake na nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.

“Hivyo natarajia kuona matunda ya semina hii kwenye mijadala mbalimbali inayoendelea hususani kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea…nashukuru sana NBC mmefanya kitu sahihi wakati sahihi,’’ alisema.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi, Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa alisema semina hiyo iliwalenga wabunge hao kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi na wenye ushawishi mkubwa kwa jamii, hususan makundi ya wanawake, ili nao wafikishe ujumbe kwa walengwa.

Akizungumiza kuhusu Chama cha wanawake Wafanyakazi wa NBC (Women Network Forum) ambacho ndicho kilichoratibu semina hiyo, Bi Lowassa alisema kinalenga kuwanganisha na pia kukuza elimu ya kifedha miongoni mwa wanachama wake ili wakawe mabalozi kwa wanawake wengine.

“Chama hiki pia kimeenda mbali kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini.Kupitia chama hiki, Benki pia imeweka utaratibu maalum wa kuwapa nafasi wafanyakazi wanawake ili kushika nafasi za uongozi.’’ Alisema huku akibainisha kuwa kwasasa benki hiyo ina wafanyakazi zaidi ya 900 ambapo asilimia 47% kati yao ni wanawake.

Katika semina hiyo ilishuhudiwa maofisa mbalimbali wanawake kutoka benki ya NBC wakitoa elimu kwa wabunge hao kuhusu mada mbalimbali za kiuchumi ikiwemo usimamizi wa fedha, mafunzo kuhusu bima za biashara na maisha na pamoja na Hati fungani ya NBC.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (Kulia – meza kuu) akifurahia pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma. Wengine ni pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa akizungumza na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake akiwemo Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (Pichani) wakichangia mada wakati wa semina hiyo.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), (wanne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati) wakati wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (wa tatu kushoto) wakati wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.

Mbunge wa Mchinga ambae pia ni mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (wa tano kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


Kwa heri! Maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya NBC, Allelio Lowassa (katikati) wakimuaga Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa wa semina ya fursa za uchumi iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya wabunge wanawake iliyofanyika leo jijini Dodoma.


No comments: