RAIS MALAWI AMPONGEZA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI KWA USHIRIKIANO KATIKA MICHEZO

 

 

 Na Meja Selemani Semunyu MALAWI

 Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera ameishukuru Tanzania kupitia  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda  kwa ushirikiano inaouonyesha  kwa nchi hiyo na jeshi lake kupitia michezo ikiwemo Gofu.

Rais Chakwera aliyazungumza hayo wakati wa sherehe za ufungaji wa mashindano ya  gofu ya kuwaenzi na kuwachangia maveterani wa vita yaliyofanyika katika Uwanja wa Gofu wa Lilongwe nchini Malawi.

“ Ninanawashuru Ndugu zetu kutoka Tanzania  hakuna nchi ambayo haipati Changamoto za kiuchumi na hakuna Nchi ambayo haipambani kutatua shinda za wananchi wake na mahitaji yao lakini kikubwa ni kusaidiana na Kuchangiana kufanikisha hilo “ Alisema Rais Nundwe.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi wa Malawi Jenerali Vicent Nundwe alisema ni heshma kubwa kwa jeshi lao kupata ugeni huo ambao umezidi kuongeza ushirikiano.

“ Najua mmesafiri kutoka Mbali kuja Malawi hii ni heshima kubwa kwetu tunawashukuru sana kwa kuacha shughuli zenu na kuja kutuunga mkono katika Mashindano haya.” Alisema Jenerali Nundwe.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mh Humphrey Polepole alisema kama Ubalozi wanamshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda kwa kuruhusu utekelezwaji wa Diplomasia kupita Michezo.

 Naye Mkuu wa Msafara wa timu ya golf ya  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo  Meja Jenerali Ibrahim Mhona alisema safari imekuwa na manufaa makubwa  kwa Majeshi ya nchi zote mbili.

Aidha Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema kwa Upande wa Klabu Baada ya Mashindano klabu sasa inajipanga kwa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara.
 
Mbali na wachezaji wa Golf Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania liliwakilishwa pia na vikundi vya sanaa kutoka Mwenge ambavyo vilitumbuiza kwa pamoja na vikundi vya sanaa kutoka Malawi.
Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera (kushoto ) akisalimiana na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kufunga Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu).Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera (kulia ) Balozi wa Tanzania Malawi Mh Humphrey Polepole (Katikati ) na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu).Rais wa Malawi Mh Lazarus Chakwera akipiga mpira wa gofu ikiwa ishara ya  kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu). 

No comments: