Benki ya NBC Yazindua Hati Fungani ya NBC Twiga Bond, kuwainua wajasiriamali na wadau wa kilimo.


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC ) imetangaza utoaji wa Hati fungani (bondi) ya miaka mitano inayofahamika kama Hati fungani ya NBC Twiga bond, ikilenga kuuza hati fungani zenye thamani ya Tsh Bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa Wafanyabiashara wadogo na wa kati, Sekta ndogo na Kilimo nchini.

Kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hiyo ni TZS 500,000 na inaweza kununuliwa kutoka tawi lolote la Benki ya NBC, au Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) wenye leseni ya udalali, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Hati fungani hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Bw Sabi alisema “Hii ni mara ya kwanza kwa Benki kutoa hati fungani kwa ajili ya umma na ikiwalenga Wajasiriamali, wakulima na wafanyabiashara wadogo ambao ndio sehemu kubwa ya ajira za vijana nchini Tanzania.’’

“Wawekezaji katika Hati fungani ya NBC Twiga Bond watapata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi.’’ Alisema.

Hati fungani ya Twiga ni ya kwanza kutolewa na Benki ya NBC na inatarajiwa kushughulikia sekta nyingine muhimu za uwezeshaji kiuchumi, changamoto ya ufadhili wa mikopo midogo midogo na ya kati nchini.

Kwa mujibu wa Bw Sabi, ofa hiyo itafunguliwa rasmi tarehe 8 Novemba 2022 na itafungwa tarehe 7 Disemba 2022. Ikishafungwa, hati fungani hiyo ya Twiga itaorodheshwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

“Hii ina maana kwamba mnunuzi wa hati fungani hiyo hiyo ataweza kuuza bondi kwa mnunuzi mwingine katika soko la pili kupitia dalali wa hisa aliyeidhinishwa na kupokea mhusika mkuu kabla ya tarehe ya ukomavu.’’ Alifafanua.

Alisema kupitia Hati fungani hiyo benki hiyo inalenga kuongeza zingine zenye thamani ya TZS 300Bn ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, Kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.

“Mapato yatokanayo na Hati fungani ya Twiga yatatuwezesha kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya makundi haya muhimu ambayo yanaajiri watu wengi. Hati fungani ya Twiga NBC iko wazi kwa umma, tukimaanisha zinaweza kununuliwa na watu binafsi, makampuni na taasisi.’’

“Ni matumaini yetu kuwa hatua hii itakuza ufanisi wa uzalishaji, kuongeza ushindani wa soko, na kutetea kanuni bora za utawala na uwajibikaji katika shughuli za biashara. Kama mnavyofahamu, sehemu kubwa ya makampuni ya biashara nchini Tanzania na duniani kote ni ya biashara ndogo na za kati (SMEs), lakini pia yanakabiliwa na mapungufu makubwa ya kifedha ambayo yanazuia ubunifu na ukuaji wa uchumi.’’ Alisema


Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwakilishi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Brighton Kinemo aliipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea mikopo nafuu kwa wajasiriamali hususan sekta ya vijana na wajasiriamali wanawake, kwa kuwashirikisha kwenye mipango mbalimbali kama vile akaunti za NBC Shambani na Kua Nasi ili kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kusaidia upanuzi wa mikopo.

“Hati fungani ya Twiga NBC inaonyesha dhamira ya benki NBC kuunga mkono juhudi za serikali kuelekea ushirikishwaji wa kifedha kwa kupanua na kuimarisha Sekta ya Fedha Tanzania kupitia utoaji wa huduma rafiki. Hii ndiyo maana halisi ya ushirikishwaji wa kifedha…hongereni sana" alisema Bw Kinemo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia) sambamba na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo wakijipongeza mara baada ya kuzindua Hati fungani (bondi) inayofahamika kama NBC Twiga Bond ya miaka mitano zenye thamani ya TZS Bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo za kilimo nchini. Hafla hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni mwakilishi wa soko la hisa la Dar es Salaam, Brighton Kinemo.

Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya NBC, Bw Theobald Sabi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hati fungani (Bondi) Inayofahamika Kama NBC Twiga Bond Ya Miaka Mitano Zenye Thamani Ya TZS Bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo za kilimo nchini.


“Hati fungani ya Twiga NBC inaonyesha dhamira ya benki NBC kuunga mkono juhudi za serikali kuelekea ushirikishwaji wa kifedha kwa kupanua na kuimarisha Sekta ya Fedha Tanzania kupitia utoaji wa huduma rafiki. Hii ndiyo maana halisi ya ushirikishwaji wa kifedha…hongereni sana"  - Brighton Kinemo, Mwakilishi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Brighton Kinemo.


Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hati fungani (Bondi) Inayofahamika Kama NBC Twiga Bond Ya Miaka Mitano Zenye Thamani Ya TZS Bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo za kilimo nchini.Hafla hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam


Baadhi ya wageni wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa hati fungani (Bondi) ya benki ya NBC Inayofahamika Kama NBC Twiga Bond Ya Miaka Mitano Zenye Thamani Ya TZS Bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo za kilimo nchini.Hafla hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam

    

Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya NBC, Bw Theobald Sabi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa  wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa hati fungani (Bondi) inayofahamika kama NBC Twiga Bond ya miaka mitano zenye thamani ya TZS bilioni 30, kwa ajili ya kupanua uwezeshaji (mikopo) wa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo za kilimo nchini.Hafla hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam




No comments: