SBL yaungana na wateja kuleta Captain Morgan Gold Tanzania


Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na walaji wa vinywaji vikali wajumuika pamoja kuzindua kinywaji cha Captain Morgan Gold na kukiingiza sokoni rasmi jambo litakalo ongozea chaguo la vinywaji vikali kwa wateja na biashara kwa bidhaa za SBL.

Uzinduzi huo wa SBL uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa The Waves, umeleta thamani katika biashara ya vinywaji vikali, kwa vile sasa kinatengenezwa ndani ya mipaka ya Tanzania tofauti na nyuma kilipo kuwa kikitengenezwa nje ya nchi.

Mkuu wa Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus, alisema kwamba kundi kubwa la walaji vijana na uchache wa bidhaa za vinywaji vikali ni kati ya sababu zilizowafanya wailete Captain Morgan Gold sokoni.

“Tafiti zinaonyesha kuwa walaji wetu makini vijana wanakosa machaguo yakutosha ya vinywaji vikali, yanayoakisi mtindo wa maisha wanaoutaka na pia vinywaji vyenye ladha nzuri na vinavyopatakana kirahisi. Captain Morgan Gold inakuja kuwa chaguo bora kwao na kulipa soko nafasi nzuri ya kuuza bidhaa inayoakisi maisha ya watu, yenye mchanganyiko wa ladha nzuri na bei poa ” alisema Bertha.

Mkuu wa Uvumbuzi aliongeza kwa kusema, “Bidhaa hii haiji sokoni kuongeza machaguo kwa walaji wetu makini nchini nzima, lakini pia kuongeza thamani katika sekta ya vinywaji kwa vile wajasiriamali watakuwa na chaguo la ziada lenye kufurahiwa na walaji kwa bei rahisi”.

Kinywaji hicho kikali, kinakuja sokoni kikiwa na historia ya utengenezaji yenye kusisimua na bei nzuri. Captain Morgan Gold itakuwa ikiuzwa kwa Tsh 5,000 kwa uzajo wa ml 200 na Tsh20,000 kwa ml 750.

Walaji wa Tanzania na wauzaji wa vinywaji vikali sasa wanajipatia nafasi ya kufurahia kinywaji chenye ubora wenye mchanganyiko wa matunda na ladha mbalimbali na zilizopikwa kwa umaridadi.

SBL inakuja kivingie katika soko la vinywaji vikali na kibunifu kushinda bidhaa zingine. Ili kufanya uzinduzi uwe wa kuvutia na maana, SBL iliwapa wateja taarifa juu ya vitu vilivyotumika kutengeneza kinywaji hicho na kuwapa walaji baadhi chupa zenye ujazo mbalimbali ili kujifurahisha na kujua ladha halisi.

Kinyaji hicho kikali kina mchanganyiko mzuri wa vanilla, sukari, matunda yaliyokaushwa na kiwango cha viungo vyenye mmea wa mwaloni, vyote vikiunganishwa kutengeneza kinywaji chenye ladha tamu.

“Uzinduzi huu unatupeleka katika nafasi nzuri, yakuwapa walaji wetu vinywaji vya kimataifa vyenye ladha yenye ubora kwa bei rahisi ” aliongeza Bertha.

SBL inachukua hatamu za kuelekea kumiliki soko la vinywaji vikali kwa mara nyingine tena kwa kuongeza chaguo pendwa katika lundo la bidhaa zake nyingi. Uzinduzi huu unafuata nyanyo za Smirnoff, kinywaji kikali kilichofanya vizuri sokoni na barani kwa ujumla.

Mkuu wa Uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bertha Vedastus (wa pili kushoto) akisubiri kuonjeshwa ladha ya kinywaji cha Captain Morgan Gold, kama ishara ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika fukwe za The Waves Jumamosi, jijini Dar es Salaam, pembeni yake ni “Manahodha na wafanyakazi” wa kinywaji hicho.

kuu wa Uvumbuzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bertha Vedastus (katikati) katika picha ya Pamoja na “nahodha”wa kinywaji cha Captain Morgan Gold katika uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika fukwe za The Waves jijini Dar es Salaam Jumamosi. Captain Morgan Gold sasa inatengenezwa na viwanda vya SBL vilivyopo nchini

Moja kati ya kundi la “Manahodha na wafanyakazi” wa kinywaji cha Captain Morgan Gold wakifurahia uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika katika fukwe za The Waves jijini Dar es Salaam, jumamosi. Captain Morgan Gold itakuwa ikitengenezwa na kupatikana nchini Tanzania.

: Mmoja wa “manahodha“wa kinywaji cha Captain Morgan Gold akifurahia uzinduzi wa kinywaji hicho katika fukwe za The Waves, uliofanyika jiji Dar es Salaam, Jumamosi. Captain Morgan Gold kwa sasa itakuwa ikitengenezwa na kupatikana nchini Tanzania.

Nadhodha wa kinywaji cha Captain Morgan Gold akifurahia uzinduzi wa kinywaji hicho kwa kukiiunua juu kama ishara ya kukileta sokoni. Tukio hilo lilifanyika katika fukwe za The Waves jijini Dar es Salaam, likiandaliwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)


Kinywaji cha Captain Morgan Gold kinatengenezwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti na kusambazwa nchini kote, mbali na hapo mwanzo ambapo kilikuwa kikitengenezwa nje ya nchi.



Baadhi ya wapenzi wa kinywaji cha Captain Morgan Gold akiwemo Mtangazaji mashuhuri Salama Jabiri (katikati) katika picha ya pamoja katika halfa ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika The Waves jijini Dar es Salaam, iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

No comments: