SBL yatangaza neema kwa wakulima Tanzania


Wakulima Tanzania wanatarijiwa kupata faida na kubadilisha maisha yao ambapo Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza mpango wako wa kununua malighafi ya mazao toka kwa wakulima wa ndani kwaajili ya uzalishaji wa bia. Kwa sasa, kampuni hiyo ya bia, inanunua takribani tani 20,000 za mahindi, shayiri na mtama kwa mwaka toka kwa wakulima wa ndani.

Akieleza zaidi juu ya azma hiyo jijini Moshi katika hafla ya ukaguzi wa kiwanda cha SBL, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma John Wanyancha, alisema kuwa kampuni hiyo inadhamiria kupanua mishipa yake ya ununuzi wa mazao toka kwa wakulima mbalimbali nchini zaidi ya mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mara na Mwanza ambayo SBL imekuwa ikinunua mazao toka mwaka 2013.

“Ongezeko la mahitaji yetu ya mazao toka kwa wakulima wa ndani ni dhumuni la makusundi la kupanua uwezo wa uzalishaji wa viwanda vyetu vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam” Wanyacha alisema, akiongezea kuwa SBL imetumia takribani billioni Tshs 165/- kwa miaka mitatu iliyopita kupanua uzalishaji viwanda vyake nchini.

Mkurungezi huyo alisema ya kuwa, wakulima wategemee kupatiwa mikataba mizuri, mbegu bure, mafunzo ya masingi ya fedha na mbinu za kisasa za kilimo kama faida moja wapo ya kufanya kazi na SBL.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu aliyepoingeza juhudi za SBL kama mdau wa maendelo nchini kupitia utoaji ajira kwa Watanzania, upanuzi wa nyenzo za maendeleo ya jamii kupitia programu zake na kuongeza mapato kwa serikali/

Mheshimiwa Babu, ambaye ni mteuzi mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro, alitembelea kiwanda hicho cha SBL na kuongea na baadhi ya wafanyakazi. SBL ina takribani wafanyakazi 800 wenye ajira ya moja kwa moja na maelefu waliopo katika mnyonyoro wa thamani ikiwemo – wakulima, wamiliki wa baa, kumbi za starehe na wasambazaji.

“SBL inasimama kidete kama mmoja wa wawekezaji makini katika uchumi na mkoa wetu (Kilimanjaro). Serikali iko makini na inaendelea kutoa ushirikiano katika kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara, ili kukuza uwekezaji na kuvutia wawekezaji zaidi kuja nchini Tanzania” Alisema Babu.

Kiwanda cha vinywaji vikali cha Moshi, kinazalisha vinywaji vyenye ubora na vilivyo zawadia tuzo kama vile, Smirnoff Extra Pure, Smirnoff Orange Zing na Bongo Don – kinywaji kikali cha kwanza cha Tanzania kilichozinduliwa na kuletwa sokoni mwaka jana.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha vinywaji vikali cha Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya upanuzi wa kiwanda hicho kilichopo mjini Moshi hapo jana.

Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) akielezea juu ya upanuzi wa kiwanda cha vinywaji vikali cha mjini Moshi, katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, iliyofanyika hapo jana.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) katika ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya upanuzi wa kiwanda cha SBL kilipocho mjini Moshi – tukio hilo lilifanyika tarehe 20 Oktoba..


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akitembelea kiwanda cha vinywaji vikali cha Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kilichopo mjini Moshi, wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa upanuzi wa kiwanda hicho hapo jana.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za kiwanda cha Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) tarehe 20 Oktoba alipotembelea kiwanda hicho cha vinywaji vikali, kama sehemu ya kufuatilia maendeleo ya upanuzi wa kiwanda hicho.

No comments: