MARATHON DAY YA ATLAS USIPIME, KUBORESHA MIUNDOMBINU YA KITUO CHA AFYA CHA FLAMINGO

Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa akifafanua jinsi Marathon Day na jinsi mbio vituo vya mbio zitakapoanzia siku ya Oktoba 14, 2022.  

Mwenyekiti wa maandalizi Siku ya Atlas (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition), Annah Lupemba akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11, 2022 wakati akitambulisha Marathon Day pamoja na uwepo wa Mahafali ambayo yataambatana na Kuenzi miaka 100 ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania akizungumza na waandishi wa hab ari jijini Dar es Salaam wakati Uongozi wa shule za Atlas walipo walipotangaza Atlas Day.


Baadhi ya Wadamini wa Atlas Marathon wakizungumza na waandishi wa habari na kueleza ushiriki wao katika siku ya Marathon itakayofanyika shule za Atlas Madale.

Viongozi wa  Atlas Mark Group na Shule za Atlas Sylivanus Rugambwa Mwenyekiti wa maandalizi Siku ya Atlas (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition), Annah Lupemba wakionesha fulana zitakazo tumika siku hiyo pamoja na Medali ambazo watatunukiwa washindi wa Mbio siku hiyo ya Oktoba 14, 2022.

SIKU ya Atlas (Atlas) kufanyika kwa namna yake ikiwa ni pamoja kuwepo na Half Marathon na Mahafali Graduation, Maonyesho ya vitu mbalimbali, michezo ya watoto na burudani kabambe.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11, 2022, Mwenyekiti wa maandalizi Siku ya Atlas (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition), Annah Lupemba amesema kuwa matukio yote hayo yatafanyika katika viwanja vya shule za Msingi na Sekondari za Madale Agosti 14, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo pia itakuwa kumbukizi ya miaka 100 ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere tangu kuzaliwa kwake kama angekua bado yuko hai.

“Katika Siku hiyo ya Atlas Day tutaanza na Atlas Half Marathon ambapo tutakua na mbio za 21km, 5km na 10km) ambazo mbio hizi zitaanzia hapa hapa katika viwanja vya shule za Atlas Madale na kuhitimishwa hapa hapa.“ Amesema Anna

Amesema kuwa lengo la kuwa na mbio hizo kwa mwaka huu ni kuboresha miundombinu ya matibabu kwa mama na mtoto katika hospital jirani ya Flamingo inayohudumia wakazi wa Madale na maeneo jirani.
 
Kauli mbiu katika mbio hizo ni "kimbia kizalendo boresha Afya" Vile vile kwa mwaka huu ambapo tarehe ya kufanyika kwa mbio yetu imeangukia siku ya kumbukizi ya baba wa taifa Mwl. Jk Nyerere Amesema kuwa kuenzi kazi nzuri alizozifanya katika taifa kwa mwaka huu Marathon yetu ina mambo mengi ambayo yataendanana yale mazuri aliyoyatekeleza kipindi cha uhai wake.

“Kwa wale wote watakaopenda kushiriki mbio hizi kwa 5km, 10km na 21km wanakaribishwa kuchangia ya ushiriki ambayo ni Tshs 30,000 kwa mtu mmoja, na kwa kikundi cha watu wasiopungua 15 basi watapata punguzo la 10% hivyo basi watachangia Tshs 27,000 tu. Na ada ya kusajili, mshiriki atapata Fulana ya kukimbilia, Namba ya kukimbilia (bib number), na pia njiani atapata huduma zoote muhimu za kukimbia kama vile Maji, Matunda, huduma ya kwanza, wrist band, na atakapomaliza mbio atapatiwa medal nzuri na viburudisho kama vile soup yenye viwango na nyama choma.” Amesema Anna

Akielezea suala la usalama kwa wakimbiaji, amesema kamati ya maandalizi imejipanga vizuri kabla na baada ya kuanza mbio kwa kupima umbali wa mbio za 5km, 10km na 21km na pia kuweka vituo vya huduma za kutosha Ulinzi wa uhakika kutoka Kiwango Security

Akimalizia amesema kuwa Usajili wa mbio siku ya Atlas Day unaendelea katika shule za Atlas yaani Atlas Primary School madale, Atlas Primary School Ubungo na Atlas Secondary School Madale na Mlimani City, ambapo katika maeneo yote hayo, Ukisha sajili tu utaondoka na kila kifaa chako cha kukimbilia siku ya Oktoba 14, 2022. Lakini pia usajili unafanyika kwa kupitia Tigo Pesa kwa kuingia katika Menu ya Tigo pesa ya *150*01# Kisha ukachagua namba 5 lipa kwa Tigo pesa, alafu ukaenda namba tano lipa ticket, hapo utachagua Marathon, alafu Atlas Marathon na kuendelea na usajili mpaka utakapokamilisha.

“Lakini pia unaweza kulipia kwa lipa namba ambayo ni Tigo 5927380. Tunapenda pia kuwahimiza washiriki wetu kwamba ni vyema wakafanya usajili na kufika kuchukua vifaa vyao mapema kwani mpaka sasa tumekwisha sajili washiriki zaidi ya 80% ambapo lengo letu ni kuwa na washiriki zaidi ya 2000.”

Pia siku hiyo kutakuwa na sherehe za Mahafali ya 17 ya shule za Atlas ambapo wanafuzi zaidi ya 700 watatunukiwa tuzo baada ya kuhitimu elimu hao ikiwa ni pamoja na wahitimu wa Nursery, Darasa la Saba na Kidato cha nne, kutoka katika shule zote Atla Primary Ubungo, Atlas Primary Madale na Atlas Secondary Madale.

Wadhamini katika Atlas Day ni Times Fm, Sharon Ringo Foundation, Maji ya Kunywa ya Afya, Kuambiana Investment, Luvanda Hardware, 2KSPORTS, Tigo pesa kwa, Montana VIP lounge, Dar Fresh, Kiwango Security, Kam na AML Finance.

No comments: