KAMPUNI YA BAKHRESA WAINGIZA SOKONI BAGAMOYO SUGER BAADA YA KUKAMILIKA AWAMU YA KWANZA YA KIWANDA CHAO


-Awamu ya kwanza kuzalisha tani 40,000, ajira zilizopatikana ni 1200

-Waishukuru Serikali,taasisi za fedha kufanikisha mradi huo


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa Ltd imetangaza kuingizwa kwa bidhaa yake mpya ya Sukari ya Bagamoyo inayofahamika Bagamoyo Suger na hiyo imetokana na kukamilika kwa Awamu ya kwanza ya mradi wa Shamba la kuzalisha.miwa linalofahamika kwa jina la Bagamoyo Suger Ltd.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Oktoba 19,2022,Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB),Hussein Sufian amesema kwamba baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza leo wanaoshuhudia uzalishaji wa sukari yenye chapa ya Azam tayari umeanza na sukari hiyo imeshaanza kusambazwa na inapatikana sokoni katika ujazo tofauti kulingana na hitajio la mwananchi.

"Tunapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia Serikali Kuu, Serikali ya Mkoa, Serikali ya Wilaya na taasisi mbalimbali za Serikali yetu ambao wamewezesha mradi huu kufika hapa ulipo kwani bila msaada huu ambao tumekuwa tunaupata kutoka idara na taasisi mbalimbali mradi huu usingeonekana.

"Mradi huu umegharimu takribani dola za Marekani milioni 110 na ni moja ya miradi ya kipekee ya kujivunia kwamba kiwango chote hicho cha fedha za gharama na mtaji zilizotumika kwenye mradi huu zimetokana na taasisi za fedha za Watanzania pamoja na kampuni yetu mama ya Said Salim Bakhresa.

"Kwa hiyo hii inaonesha inawezekana kuwa na miradi mikubwa ya kimkakati inayoweza ikafadhiliwa na taasisi za fedha za ndani kama ambavyo mradi huu wa Bagamoyo Suger ulivyoonesha hilo, kwa kweli nichukue nafasi hii kwa kipekee kabisa kuzishukuru taasisi za fedha ambazo tunashirikiana nazo kwa kuhakikisha tunapata fedha za kutosha kwa ajili ya kuanzisha mradi huu mpaka hapo ulipofikia awamu hii ya kwanza,"amesema.

Akieleza zaidi, Sufiani amesema bidhaa wanayoizungumzia ya Sukari ya Bagomoyo Suger wameifungasha kulingana na mahitajio la wateja wao."Tunamfuko wa kilo 50 ambao unapatikana sokoni, tuna mfuko wa kilo 25 ambao pia uko sokoni ,tuna mfuko wa kilo moja na pia tuna gramu 320 na gramu 150.

"Lengo ni kuona wananchi wanaweza wakapata bidhaa kwa ujazo tofauti kulingana na mahitajio yao lakini pia kupitia Idara ya Masoko wanaendelea kupokea maswali mbalimbali ya namna gani wanaohitajia sukari hiyo wanaweza kuipata ,kwani kwa kiwandani haizuzwi kwa mtu mmoja mmoja bali wanauza kwa wasambazaji ,"amesema

Aidha amesema wanawashukuru watu wote ambao wanaamini ni wateja wao kwani kama hukutumia bidhaa moja basi utaenda kutumia bidhaa nyingine ya Bakhersa.hivyo wanawashukuru kwa kutumia bidhaa zao bora na sasa pia wanawakaribisha waendelee kutumia bidhaa yao mpya.

"Na sisi tunamsemo wetu tunasema maisha matamu na Bagamoyo Suger, kwa hiyo unaweza kunywa chai sasa hivi na sukari ya Azam , wakati ukiwa unakula mkate, chapati au kitumbua ama donati iliyotengenezwa na unga wa Azam wakati huo huo ukiangalia morning trampet ukijiandaa,"amesema.

Kuhusu ajira zilizopatikana baada ya kukamilika Awamu ya kwanza ya mradi huo amesema ni ajira 1200 , na uwezo wa uzalishaji kwa awamu ya kwanza ni tani 40,000 , hivyo watakapokamilisha Awamu ya pili wanatarajia kufika mpaka tani 80,000 kwasababu wataongeza hekta 2000 kwa kila awamu ambayo inakupa wastani wa sukari tani 40,000 na Awamu ya tatu wanatarajia kuwa na tani zaidi ya 100,000.

Kuhusu awamu nyingine amesema itategemea na upatikanaji wa maji kwani kwenye eneo lao huwezi kulima mua mpaka umwagilie lakini wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanapata maji ya kutosha."Kwanza kuweza kumudu hili eneo ambalo tunalo ili ulime miwa tnahitaji maji ya kutosha ili tuweze kufanya upanuzi.

"Kwa hiyo hatuwezi kutoa muda kamili tutaanza mwakani au lini awamu zilizobakia kwasababu huu ni mchakato ambao watalaamu wapo na wanafanyia kazi,lakini katika michoro ya uwekezaji hizo awamu hizo zipo , kutakuwa na Awamu ya pili na ya tatu."

Alipoulizwa iwapo wanaweza kutumia maji ya bahari ya Hindi kwa kusafisha maji na kuyatumia kumwagilia amesema ni kweli teknolojia hiyo ipo lakini sio kwa matumizi ya shamba na gharama yake ni haiwiani na hicho wanachokipata na sukari hiyo hatuwezi kuiuza.

Kuhusu uhaba wa sukari nchini amesema watakapokamilisha awamu zote kunaweza kuwa na sukari ya kutosha lakini kama nchi Ina mikakati yake wa kujitosheleza kwa sukari yake ya ndani, kwa hiyo kina miradi mingine mipya, sio mradi wao peke yao.

"Kuna miradi mingine mipya inaendelea kwa mujibu wa takwimu ambazo zinazo ninafahamu itakapofika mwaka 2025 nchi yetu imejiwekea lengo la kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 700,000 ambazo zitatosheleza mahitaji ya Sukari ya ndani na naamini hilo litafikiwa.Kwasababu kuna miradi mbalimbali na huenda mradi huu Awamu pili utakuwa umeshaanza.

Kuhusu umeme Sufiani amesema hawana changamoto ya umeme na kufafanua eneo hilo liko pembezoni kidogo hivyo kuna laini imejengwa kutoka barabara kubwa hadi kwenye eneo la mradi.Aidha moja ya sehemu ya kiwanda ni kuzalisha umeme unaotokana na taka za miwa.

" Kwa hiyo tunao uwezo wa kuzalisha megawati tano na matumizi ya kiwanda ni megawati 3.5 lakini itategemea na mahitaji ya matumizi ya kiwanda. Kwa hiyo tuko katika mchakato wa kukamilisha makubaliano na TANESCO kwamba kiwango cha umeme uliozidi tutaupeleke katika gridi ya Taifa ili uweze kuwafaa watumiaji wengine wa maeneo yanayotuzunguka.Hivyo sisi tunashukuru hatuna changamoto ya umeme,tunatumia umeme wetu wenyewe tunaozalisha," amesema Hussein.


Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB),Hussein Sufian akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sukari inayozalishwa katika kiwanda cha Bagamoyo Sugar kilichopo kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya kukamilika kwa Awamu ya kwanza ya mradi wa Shamba la kuzalisha miwa linalofahamika kwa jina la Bagamoyo Suger Ltd.





Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB),Hussein Sufian akifafanua mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hatua ya kuingizwa sokoni kwa bidhaa yake mpya ya Sukari ya Bagamoyo inayofahamika Bagamoyo Suger kutokana na kukamilika kwa Awamu ya kwanza ya mradi wa Shamba la kuzalisha miwa linalofahamika kwa jina la Bagamoyo Suger Ltd. kilichopo kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR


Waandishi wa Habari wakitazama makala maalum ya kiwanda hicho


Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB),Hussein Sufian akizungumza jambo kwa Wwaandishi wa habari (hawapo pichani) iliopo sehemu ya mitambo ya kuvuna maji na kiasi cha maji kilichopo inayotumika katika kiwanda cha Bagamoyo Sugar kando ya mto Wami.




Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB),Hussein Sufian akifafanua namna Mitambo inavyotumika kusambaza maji kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mashamba ya miwa
Mhandisi wa Umwagiliaji katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar Steven Peter akieleza namna mitambo inavyotumika kuchanganya kemikali ikiwemo mbolea kwa ajili ya kumwagilia mashambani

Mhandisi wa Umwagiliaji katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar Steven Peter akieleza namna mitambo ya umwagiliaji katika kituo cha umwagiliaji mashamba inavyo fanya kazi.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR



Mitambo ya uvunaji miwa ikivuna miwa tayari kupelekwa kiwandani kuchakatwa kwa ajili ya kuzalisha sukari


Naibu Mkurugenzi Kiwanda cha Kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar,Said Nassor akitoa maelezo ya awali kabla ya kuelekea kwenye kiwanda kuona namna Sukari inavyotengenezwa

Shehena ya miwa ikipimwa uzito kwenye eneo maalum na la kisasa kabisa

Shehena ya Miwa ikiwa tayari kwa ajili ya kuchakatwa

Naibu Mkurugenzi Kiwanda cha Kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar,Said Nassor akitoa maelezo katika eneo la kupokelea miwa kwa ajili ya uchakataji kabla ya kuzalisha sukari katika kiwanda hicho.






Eneo linalozalisha umeme,ambapo Megawati 5 zinazalishwa kwa ajili ya kutumia kuendesha mitambo kiwandani hapo, kiwanda hicho kinatumia megawati 2 kwa uzalishaji.


Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika eneo la mwisho la kufunga sukari mara baada ya kuzalishwa kiwandani hapo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakitazama sukari ambayo tayari imezalishwa kiwandani hapo na tayari kuingizwa sokoni,PICHA ZOTE NA MICHUZI JR

No comments: