WANAFUNZI WANAOTEGEMEA KUFANYA MITIHANI YA BODI YA NBAA WAPIGWA MSASA
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imewakutanisha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972.
Akizungumza leo wakati wa kufungua Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu amesema leo wamekua na kikao cha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi katika ngazi mbalimbali ikiwa na lengo la kuwanoa kwenye mbinu mbalimbali za mitihani hasa kwenye maeneo yanayokuwa na changamoto kubwa sana kwa watahiniwa wa Bodi.
Amesema yapo Masomo yanaleta changamoto Sana na kiwango cha ufahulu unakuwa mdogo hivyo tumewaletea walimu wa Masomo hayo kutoka vyuo na Taasisi mbalimbali ili waweze kuwapa uzoefu wao na kuwapa mbinu mbalimbali za kuweza kujiandaa na mitihani ya Bodi.
"Tumewasisitiza Sana namna ya kujiandaa wasijiandae kiholelaholela bali waweke muda wa kutosha kwenye kujifunza kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya watahiniwa wa vyuo na watahiniwa wa mitihani ya Bodi " alisema Temu
Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufahulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na ukaguzi.
Naye Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo anasema Bodi hiyo imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mtahiniwa anafanya mitihani ya Bodi hiyo na kuhakiksiha wanaondoa changamoto zote.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu akizungumza na watahiniwa
wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972 ambapo kilele chake ninatarajiwa kufanyika Novemba 28, 2022.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo akizungumza jambo pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu kwa ajili ya kufungua kikao kazi cha watahiniwa
wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972
Afisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Humphrey Symphorian akizungumza jambo kwenye semina ya watahiniwa wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972
Baadhi wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi, Wakufunzi pamoja na wafanyakazi wa Bodi wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Profesa Sylvia Temu wakati wakufungua semina kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo Mwezi Novemba mwaka 1972 iliyofanyika kwenye ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Semina ikiendelea
Picha ya pamoja
No comments: