USHIRIKIANO HAFIFU WASABABISHA WAFANYAKAZI SEKTA ZISIZO RASMI KUTOJIUNGA NA MIFUKO YA JAMII
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam. Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi wakati akitoa tathmini ya utafiti wa alioufanya. katikati ni Mkuu wa idara ya Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara ndogondogo “VIBINDO”, Gaston Kikuwi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam. Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza wakati alipokutana na Vingozi wa Asasi za Kirai, NSSFpamoja na NHIF katika chuo kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Septemba 8, 2022.
Mkuu wa idara ya Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge akizungumza wakati wa kufunga kikao ch tathmini ya utafiti uliofanywa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Godbertha Kinyondo juu ya bima za afya na mifuko ya kijami kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara ndogondogo “VIBINDO”, Gaston Kikuwi.
Baadhi wa viongozi wa asasi za kiraia wakichangia mada katika kikao kilichofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Septemba 8, 2022.
Picha ya pamoja.
TATHMINI imeonesha kuwa bado kuna idadi ndogo ya wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi ambao wamejisajili katika mifuko ya hifadhi za kijamii kutokana na changamoto mbalimbali haswa ushirikiano hafifu baina ya sekta zisizo rasmi na mifuko hio.
Hayo yamedhihirika katika kikao cha Kikao cha usambazaji na kufanya tathmini ya matokeo ya utafiti unaohusiana na hifadhi za kijamii katika sekta zisizo rasmi, kilichoshirikisha mashirika ya kiserikali
Mfuko wa bima ya afya ya taifa(NHIF) na Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) pamoja na Vyama vya wafanyakazi, Chama cha wamiliki wa magari ya abiria, Jumuisho la vyama vya wafanyabiashara ndogo ndogo, vyama vya usafirishaji kama wadau mojawapo wa sekta zisizo rasmi.
Kikao hicho kimefanyika Septemba 8, 2022 Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam. Kilichoongozwa na Mhadhiri wa chuo hicho Ndaki ya Dar es salaam, Dkt. Godbertha Kinyondo
Mkaganyiko katika sera na sheria za nchi za huduma hizo, imeonesha kuwa hazitabiriki kwa mabadiliko katika huduma hizo.
Pia imeonesha kuwa uelewa hafifu wa wanufaikaji kuhusu bima ya afya na Pensheni za uzeeni.
Mkutano huo uliazimia kuimarisha ushirikiano wa dhati baina ya mifuko ya hifadhi za kijamii Pamoja na uongozi wa vikundi vya wajasiriamali na wafanyakazi katika sekta zisizo rasmi ambao ni daraja kuu la kuwafikia kirahisi na pia kama usajili na dhamana rasmi ya wanakikundi wao na hivyo kuondoa vikwazo vikuu kwa wanachi wa kawaida katika kufaiidi huduma hizo.
Akizungumzia mifuko hiyo Dkt. Kinyondo amesema Mifuko hiyo ilionesha kuwa katika mchakato wa kuhakikisha watu wa sekta zisizo rasmi wanaingizwa katika sekta hizo kwa kuwatengenezae vifurushi na huduma ambazo zinaendana na mazingira na hali zao halisi.
Kwa upande wa wajumbe wa NHIF walitoa rai vikundi kujiepusha vitendo vya kutokuwa waaminifu haswa kwa kuwaruhusu mamluki kujisajili na vikundi hivyo pindi wanapokuwa na shida ya huduma za haraka na hivyo kupelekea gharama za uendeshaji wa Mfuko wa afya kuwa mkubwa kuliko makusanyo na hivyo mifuko hiyo kushindwa kutekeleza mikakati ya kuwapatia huduma zao kwa muda mrefu Zaidi.
“Changamoto tulioipata tulipokuwa na vikundi vya watu kumi kumi ni (Kikoa), walikuwa wakichanga 76,000 kwa kila mmoja, mpango huu ulishindwa. Kutokana na l matumizi kuwa makubwa kuliko mapato tuliokusanya na hivyo mfuko huu ukashindwa kuwa endelevu, kwa sababu tulikuwa tukitegemea fedha kutoka makundi mengine kama watumishi wa Umma.
Na uwepo mkubwa wa mamluki unaochangiwa na viongozi kutokuwa waaminifu lakini pia ufa katika sehemu ya usajili na ndio maana kwa sasa tunahitaji vikundi vyenye mlengo mmoja wa shughuli ya kiuchumi kama bodaboda, daladala, mama ntilie na kadhalika” Alisema Thomas Mkusa
Lakini Pia Mkuu wa mradi huo, Dkt Kinyondo alitoa rai kwa viongozi wa vikundi hivyo, kutoa mrejesho na kuwashirikisha wanachama kwa kila wanayojifunza kutokana na vikao na mafunzo ya mradi huo ili kuwafikia na kuwabadili wahusika wengi zaidi lakini pia kwa mifuko ya hifadhi Za kijamii, kuweka taratibu na nguvu Zaidi katika sekta zisizo rasmi kuliko kutegemea wanachama waliopo katika ajira rasmi ambao ni wachache na hivyo kufanya Mifuko hiyo kutokuwa na manufaa makubwa zaidi kwa wananchi wengi.
Na hii inasababisha kupoteza mapato mengi ambayo wangeyapata katika sekta zisizorasmi.
Kwa upande wa washiriki wametoa rai kuwa machapisho ya matokeo ya tafiti kikiwemo kitabu kilichochapishwa tayari na kipo mtandaoni, yatolewe katika lugha ya Kiswahili ili yawanufaishe watu wengi wenye nia ya kusoma matokeo ya tafiti huo.
Aidha tathmini imeonesha kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo kutoka Kenya wana bima za afya na wafanyabiashara ndogo ndogo hapa nchini hawana bima za afya.
Akizungumzia Mkakati wa utafiti uliofanywa unlionesha kuwa walengwa ili waweze kuwaingiza wanachama wao katika kupata hifadhi za jamii ni lazima kutolewe ilimu ya kutoka kutoka katika mifuko ya hifadhi za jamii na bima ya afya nchini.
Dkt.Kinyondo ameahidi kuwa kusambaza matokeo ya tafiti hiyo, ili ikawafikie wafanyakazi wasio rasmi ili waweze kushiriki katika kupata huduma hizi maridhawa.
"Na sisitiza mahusiano ya taasisi na vyama vya wafanyakazi maana hawa wapo nao, na wengi wa viongozi ni wafanyakazi hizo ndogo ndogo maana wanafahamu fika changamoto na mafanikio ya watu wanaowaongoza." Amesema Dkt. Kinyondo
No comments: