TUMIENI MAWASILIANO KUJIIMARISHA KIUCHUMI- Mhandisi Asajile John
Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano Mabel Masasi akitoa maelezo kuhusiana na matumizi ya simu kwa kujiletea maendeleo na namna ya kutumia kwa usalama wa mtandaoni kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na Viunga vyake mkoani Njombe.Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akizungumza na wananchi kuhusiana na matumizi ya simu kwa maaendeleo ya uchumi wakati wa Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na viunga vyake mkoani Njombe.
Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano Mabel Masasi akizungumza na mwananchi kuhusiana na matumizi ya simu na namna ya kuwa makini na matumizi ya simu wakati TCRA ikiwa katika utoaji wa elimu kwa wananchi katika mikusanyiko kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na Viunga vyake mkoani Njombe .
Picha za matukio mbalimbali kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako ambapo TCRA ikiwa inatoa elimu juu matumizi salama ya simu na kutumia simu kwa katika maendeleo ya kiuchumi.
Picha za matukio mbalimbali kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako ambapo TCRA ikiwa inatoa elimu juu matumizi salama ya simu na kutumia simu kwa katika maendeleo ya kiuchumi.
Wananchi wa Makambako wameshauriwa kutumia huduma za mawasiliano kujiimarisha kiuchumi ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika Gulio la wiki lililofanyika katika eneo la Soko Kuu la Makambako Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John amesema mawasiliano yamerahisisha upatikanaji wa fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.
Mhandisi Asajile amesema katika Ulimwengu wa sasa taarifa nyingi za uboreshaji wa huduma, biashara, masoko na kilimo zinapatikana mtandaoni na kuwataka wananchi wa makambako kutumia fursa hizo.
Ametoa mfano wa taarifa za uboreshaji wa kilimo, upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo na misitu pamoja kutangaza bidhaa katika masoko ya ndani na ya kimataifa kuwa zinaweza kupatikana mtandaoni na kuwasihi wananchi badala ya kutumia mitandao kufanya mambo yasiyo na faida wajielekeze katika maeneo hayo ya msingi
Huu ni muendelezo wa kampeni ya kuelimisha umma juu ya matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano ijulikanayo kama kwea kidijitali inayoendeshwa na TCRA nchi nzima.
No comments: