Nape: Tunahitaji Wazalishaji wa Maudhui Kuzalisha kwa ubora
Picha ya pamoja wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).*TCRA yajikita katika uchumi wa kidijitali unaokwenda sambamba na maudhui
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amewataka wadau wa Uzalishaji na usambazaji wa maudhui kuweka mikakati itakayosaidia nchi kuzalisha na kuandaa maudhui bora yakayoweza kushindana katika soko la utandawazi kwa kutumia Lugha ya Kiswahili.
Maudhui yakitumia lugha ya kiswahili yanakuwa bora na kuweza nchi nyingine kuchukua na kuongeza uchumi wa nchi yetu kama nyingine zilivyoweza kufanya hivyo na sisi tukachukua huko
Waziri Nape ameyasema katikka katika mkutano uliowakutanisha wadau wa uhamasishaji uandaaaji na usambazaji wa maudhui nchini.
Alisema ni ukweli usiopingika kuwa mabadiliko ya teknolojia ya habari na utangazaji yameipeleka nchi katika duniani nyingine ambayo maudhui yake hayana mipaka kutokana na teknolojia ndiyo inakwenda kwa kasi ambapo wadau wa maudhui hayo ni wakati wa kuzalisha maudhui bora.
"Teknolojia haitambui mipaka yetu tuliojiwekea kwa sasa unaweza kupokea maudhui yoyote ilimradi uwe na kifaa cha kuyapokea maudhui hayo.amesema Nape.
Amesema kampuni kubwa za kimataifa zimekuwa zikishindana kutengeneza na kusambaza tamthilia na katuni za watoto, vichekesho.
Alisisitiza kuwa ni wajibu wetu kutumia teknolojia iliyopo kuhakikisha tunaingia katika ulimwengu wa ushindani na utandawazi ambao utaweza kuvutia Watanzania na watazamaji kuweza kutagaza utamaduni na hatimaye kuongeza pato kwa Taifa na kufungua fursa ajira.
Nape aliishauri Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kuandaa tuzo ya mzalishaji bora wa maudhui ya ndani ili kuongeza ushindani katika soko.
Pia amewataka kuweka kanuni ambazo zitasimamia wazalishaji binafsi wa maudhui ili kuwawezesha kuuza kazi zao katika soko la nje.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Habi Gunze alitaja baadhi ya changamoto zilizobainika kwwnye uzalishaji wa maudhui ni uhaba wa mitaji, mitaala kupitwa na wakati, ukosefu wa mafunzo kwa wabunifu.
Alitaja changamoto nyingine ni kutotengwa muda wa kutosha wa kuonesha maudhui ya ndani kwani asilimia 68 ya maudhui hasa ya tamthilia za kigeni zimekuwa zikionesha maudhui ya kimapenzi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk.Bakari Jabiri alisema mamlaka hiyo katika mpango kazi wake umejikita kukuza maudhui ya ndani na uchumi wa Kidigitali.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na waandishi wakati akifungua mkutano wa wadau wa uzalishaji wa maudhui, jijini Dar es Salaam. wa maudhui nchini jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Habbi Gunze akizungumza kuhusiana na maudhui yanayozalishwa nchini katika mkutano wa wadau wa uzalishaji wa maudhui jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk.Jabiri Bakari akizungumza kuhusiana na TCRA ilivyoweka Mikakati ya kukuza uchumi wa kudijitali katika mkutano wa wadau wa uzalishaji
Picha ya pamoja wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Picha ya pamoja wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa na Jumuiya ya waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (Jumikita )
Picha ya pamoja wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa na Wahadhiri wa Vyuo vya Uandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa na Sektretarieti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyofanikisha mkutano wa wadau.
No comments: