Halmshauri za jiji la Dar es Salaam zaagizwa kutekeleza afua za malezi ya Mtoto
Mkuu wa Wilaya ya Kinondono Godwin Gondwe akiwa na wadau wa ukatili wa watoto mara baada ya kuzindua program ya ulinzi wa mtoto ngazi ya mkoa wakati alipomwakilisha mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
HALMASHAURI za Mkoa wa Dar es Salaam zimetakiwa kutekeleza afua za Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) Ili watoto waweze kukua Katika utimilifu wa mwili na akili.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Amos Makala wakati wa uzinduzi wa Programu hiyo Kwa ngazi za Mkoa.
Gondwe alisema kuwa, watoto wanahitaji kulelewa Katika mazingira Bora Ili waweze kuimarisha afya ya mwili na akili, jambo ambalo litasaidia kuboresha ukuaji wa ubongo wao na kupata viongozi Bora wa baadaye, hivyo basi Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha kuwa, afua hizo zinatekelezwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu Kwa Wananchi Ili waweze kuzielewa na kuzitekelza Kwa vitendo.
" Kila halmashauri inapaswa kutekeleza afua za Programu jumuishi ya Malezi, makuzi na maendeleo ya Awali ya Mtoto, lengo ni kuhakikisha kuwa watoto wanakuja Katika mazingira Bora ambayo yatamjenga Katika ukuaji wake, hivyo basi Kila mmoja an wajibu wa kutekeleza afua hizo Kwa vitendo," alisema Gondwe.
Aliongeza kuwa, vitendo vya ukatili vina uojitokeza Katika jamii ni pamoja na wazazi au walezi kushindwa kutimiza wajibu wao Katika Malezi, jambo ambalo limesababiaha kukithiri kwa vitendo vya ukatili Katika jamii zetu.
" Kuna vitendo vya ukatili wa aina mbalimbali za Katika jamii zetu ikiwamo ulawiti,ubakaji na utesaji ambao unafanywa na ndugu wa karibu wa watoto kutokana na maslahi Yao binafsi, hivyo basi Serikali haitawavumilia watu hao Kwa sababu inachangia kiwalea watoto Katika mazingira hatarishi,tutawwchukulia hatua Kwa mujibu wa sheria Ili iwe fundisho wa wengine," alisema.
Aliongeza kuwa, mkakati wa Mkoa ni kuhakikisha wanashirikiana na wadau mbalimbali Kwa ajili ya kutoa elimu Kwa Wananchi Ili kupunguza vitendo hivyo.
No comments: