BENKI YA NMB YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA MKOANI TABORA

 Benki ya NMB inaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuhakikisha wanazielewa bidhaa na mipango ya benki hiyo ili wanufaike na biashara zao.

Akizungumza katika warsha ya klabu ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Tabora, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese,alisema kikao na wafanyabiashara ni muhimu katika kubadilishana mawazo.

Magese alisema warsha hio ambayo haijafanyika tangu mwaka 2019 kutokana na ugonjwa wa UVIKO19, imekuwa na mafanikio makubwa kwa pande zote mbili na kuongeza kuwa wamepata fursa ya kuwaeleza wafanyabiashara bidhaa zao ikiwemo riba ya asilimia tisa katika kilimo.

Alieleza kuwa Benki ya NMB imechukua changamoto zote zilizotolewa na wafanyabiashara hao na kuahidi kuwa benki hiyo itazifanyia kazi haraka.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya wafanyabiashara hao,Michael Mambo,aliwataka wafanyabiashara kuacha uoga wa kukopa kutoka taasisi za fedha huku akisisitiza kuwa mikopo ina manufaa makubwa na iheshimiwe huku akiwasihi kutoitumia kinyume na malengo waliyokusudia.

Mfanyabiashara Elizabeth Nkonyoka alisema wamefurahi na kunufaika na warsha hiyo kwa kupata elimu ya kifedha na kujua masuluhisho mbalimbali ya kifedha ikiwemo umuhimu wa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa wamenufaika na bidhaa za benki NMB na kushauri kuwa warsha kama hizo ziwe zinafanyika kila mwaka angalau mara moja.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese akizungumza na wafanyabishara wa Mkoa wa Tabora.
Mwenyekiti wa Klabu ya wafanyabishara Mkoa wa Tabora, Michael Mambo akifungua warsha hiyo iliyofanyika Mkoani Tabora.
Wafanyabishara katika warsha ya klabu ya wafanyabishara Mkoani Tabora iliyoandaliwa na benki ya NMB

No comments: