BENKI YA NCBA YAKABIDHI ZAWADI YA PIKIPIKI KWA WASHINDI WA KAMPENI YA MPAWA.


 Benki ya NCBA imekabidhi zawadi ya pikipiki tatu kwa washindi wa awali wa kampeni ya Mpawa ijulikanayo kama, chuzi limekubali iliyoanza mwezi Agosti mwaka huu katika viwanja vya soko la Mabibo.

Kampeni hio inafanywa kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Vodacom ambayo imelenga kuwahamasisha watanzania kuweka akiba ili kujihakikishia fedha zaidi katika akaunti zao.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kitengo cha fedha kutoka NCBA, Genesi Kunda alisema kuwa huduma ya Mpawa imekuwa mstari wa mbele kuwasaidia watanzania kwa muda mrefu kupata mikopo ya haraka na kwa riba nafuu sana.

Alinukuliwa, ‘Kampeni hii imelenga kuhamasisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuweka akiba ya fedha zao kupitia huduma ya Mpawa ambapo pia wataweza kupata mikopo ya haraka na kwa riba nafuu kuliko sehemu au huduma zingine zozote’.

Aidha, Kunda aliendelea kuzungumzia kampeni hio ilivyoleta motisha kwa wateja kwa kuzungumzia zawadi ziliziopo.

Alisema, ‘tunatoa fedha taslimu shs 50,000/= kwa wateja wanaorejesha mikopo yao ndani ya siku sita. Kila wiki kuanzia wiki hii tumewazadia wateja hamsini waliorejesha mikopo yao mapema na kuweka akiba.

‘Tunazidisha mara mbili ya Akiba aliyohifadhi Mteja kwa wateja miamoja (100) kila mwezi. Wale wataokaoweka akiba na sisi kipindi hiki cha kampeni watakuwa na nafasi ya kubahatika kushinda mara mbili ya Akiba yao kila mwezi. Weka kuanzia shilingi elfu kumi.

‘Tutatoa zawadi kubwa kuliko zote mwishoni mwa kampeni yetu kwa wateja wote watakaoweka akiba na sisi na kuchukua mkopo na kufanya marejesho kwa wakati ndani ya siku sita, watakuwa na nafasi ya mmoja wao kuibuka na ushindi mnono wa fedha taslim milioni Tano mwishoni kabisa mwa kampeni’.

Benki ya NCBA imepanga kuhakikisha kuwa kampeni hio kuwa endelevu katika kuhamasisha ukuaji uchumi kwa mtu mmoja mmoja hasa wafanyabiashara kama wamama ntilie, waendesha bodaboda, bajaji, wamachinga na wengineo.

Annastazia Yenze kutoka Morogoro, mmoja wa washindi aliipongeza kampeni hiyo ambayo imemtia moyo katika kufanya shughuli zake za kilimo. Alinukuliwa, 'Nimefurahi kushinda pikipiki hii; itanisaidia sana kama mkulima katika kusafirisha mazao yangu sokoni. Ningependa kuishukuru Benki ya NCBA kwa kampeni hii.'

Kwa upande mwingine, Salome Kapela na Ibrahim Nzunda kutoka jijini Dar es Salaam ambao waliwahi kudhani kuwa haiwezekani kushinda, walijawa na furaha baada ya kupokea pikipiki hizo, wote wakitoa shukrani na kuwataka wananchi kushiriki katika kampeni ya Mpawa.

Hadi sasa huduma ya Mpawa ina wateja zaidi ya milioni 6 nchini kote wanaonufaika na mikopo midogo isiyokuwa na kima cha chini mpaka laki tano wakiwa ndani au nje ya Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya NCBA, Genesi Kunda (wa pili kulia), akiwakabidhi washindi watatu zawadi za kila wiki ya pikipiki katika viwanja vya soko la Mabibo wakati wa kampeni ya Mpawa inayohamasisha wateja kuweka akiba, kukopa na kurejesha mikopo mapema ili kujishindia zawadi bora za kila wiki katika kampeni ijulikanayo kama‘Chuzi. Limekubali' kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom. Wa kwanza kushoto ni Jackson Maka akipokea zawadi kwa niaba ya Salome Kapela, akifuatiwa na Ibrahim Nzunda na wa kwanza kulia ni Annastazia Yenze.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya NCBA, Genesi Kunda (wa pili kulia) katika viwanja vya soko la Mabibo, akimkabidhi zawadi ya pikipiki Jackson Maka (kushoto) kwa niaba ya Salome Kapela, mmoja wa washindi watatu wa pikipiki za kila wiki kutoka NCBA kwa kushirikiana na Vodacom katika kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la, "Chuzi Limekubali", ambayo inalenga kuhamasisha watu kuweka akiba na kukopesha kwa kurejesha mikopo mapema. Kulia kabisa ni Annastazia Yenze kutoka Morogoro, mshindi mwingine wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya NCBA, Genesi Kunda (wa pili kulia) akiwa katika viwanja vya soko la Mabibo, akimkabidhi zawadi ya pikipiki Ibrahim Nzunda (wa pili kushoto), mmoja wa washindi watatu wa pikipiki za kila wiki kutoka NCBA kwa kushirikiana na Vodacom katika kampeni ya Mpawa iliyopewa jina la, “Chuzi. Limekubali", ambayo inalenga kuhamasisha watu kuweka akiba, kukopa na kurejesha mikopo mapema kujishindia zawadi. Kulia kabisa ni Annastazia Yenze kutoka Morogoro, na kushoto kabisa ni Jackson Maka kwa niaba ya Salome Kapela, washindi wa tuzo za kila wiki za pikipiki wakitokea jijini Dar es Salaam.


Mshindi kutoka Morogoro, Annastazia Yenze (kushoto) akikabidhiwa zawadi yake na Genesi Kunda (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Fedha kutoka NCBA.


No comments: