WAUZAJI WA REJAREJA WA YARA KUJISHINDIA ZAWADI KABAMBE KUPITIA KAMPENI YA MAUZO
KAMPUNI ya Mbolea inayoongoza nchini ya Yara Tanzania, leo imekabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni inayoendelea ya programu ya uaminifu iitwayo YaraConnect. Katika tukio la leo muuzaji wa rejareja wa mjini Lushoto, Bwana Hussein Kaniki, mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet alizawadiwa pikipiki mpya aina ya Boxer 150-UG yenye thamani ya shs milioni tatu.
Akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi, Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara Tanzania, Deodath Mtei alisema “Kaniki Agrovet alijikusanyia pointi 33,333 katika mauzo ya bidhaa za Yara na kisha kupiga picha stika maalumu zinazowekwa juu ya mifuko wakati akiuza bidhaa kwa wakulima. Muuzaji rejareja huyu akatumia pointi hizi kujishindia pikipiki yenye thamani ya shs milioni tatu”.
Akaongeza kwamba progamu hii huwapa pointi za uaminifu wauzaji wa rejareja wanaponunua ama kuuza bidhaa za mbolea ya Yara ambazo zinaweza kutumika kupata zawadi za pesa taslimu ama zawadi zisizo za fedha. “Kwa kuskani msimbo (stika) maalumu (QR code) zilizowekwa juu ya mifuko wakati wa kufanya mauzo ya bidhaa kwa wakulima, muuzaji wa rejareja anajikusanyia pointi ambazo anaweza kuzitumia katika kujishindia pikipiki ama zawadi nyingine ikiwa ni pamoja na kofia, fulana, chupa za chai, makoti, simu za mkononi aina ya infinix, chupa za maji na pesa taslimu hadi kiasi cha shs 3,600,000”.
Akawataka wauzaji wa rejareja wote kuchangamkia fursa hii kupata taarifa zaidi kuhusu bidhaa za Yara na pia kujishindia zawadi. “Kampuni imetenga mamilioni ya shilingi kuwezesha programu hii na tutaendelea kuleta masuluhisho mengine ya kidigitali ili kuhakikisha wadau wetu wanafanikiwa,” alisema.
Kwa upande wake Bwanashamba Mauzo wa Yara Kanda ya Kaskazini, Novatus Salala alisema ndani ya programu ya YaraConnect kuna eneo lenye video za maarifa na taarfia kuhusu matumizi bora na sahihi virutubisho vya mazao. Muuzaji wa rejareja anaweza pia kupata taarifa zitakazoweza kuwasaidia wakulima kutatua matatizo ya ukosefu wa virutubisho unaoathiri uzalishaji lakini pia kuweza kusimamia akiba zao vizuri.
Akizungumza muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Bwana Kaniki alisema anayo furaha kubwa na kuishukuru Yara kwa msaada wao na kwa kuwakumbuka wauzaji wa rejareja. “zawadi hii imenipa hamasa kubwa, naishukuru Yara kwa kuendelea kujitolea kuwasadia wauzaji wa rejareja. Nitaendelea kuuza bidhaa za Yara kwa bidii nyingi na natoa wito kwa wauzaji wengine kujiunga na YaraConnect”, alisema Bwana Kaniki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Yara, Bwana Winstone Odhiambo naye alisema kampuni itaendelea kuhakikisha kunakuwa na mbolea bora, ya kutosha na yenye bei nafuu katika soko. Akiukaribisha mpango wa mbolea ya ruzuku ya serikali akisema utasaidia sana katika kuhakikisha wakulima wanapata ahueni kutoka katika makali ya sasa ya bei.
Bwana Odhiambo anasema; Wauzaji wa rejareja wa Yara wana kila sababu ya kuwa na uhakika wa msaada na ushirikiano wetu endelevu katika kuhakikisha bidhaa zetu zote zinapatikana kwa wakati katika soko. Programu ya YaraConnect ni moja ya juhudi za kampuni katika kuwatambua na kurudisha shukurani kwa wateja wetu wa thamani.”
Programu yara Connect ilizinduliwa Julai 1, 2021 ikiwa na lengo la kutoa msaada wa kiufundi kuhusu masuala ya kilimo na matumizi bora ya mbolea za Yara, kuwapa wauzaji wa rejareja kujifunza na kupata majibu ya maswali kuhusu kilimo na matumizi sahihi ya bidhaa za Yara na pia kupata msaada kwa mteja kupitia program hiyo.
Programu inapatikana kote kupitia play store kwa watumiaji wa simu za android ama apple store kwa watumiaji wa IOS. Kwa taarifa zaidi wauzaji wa rejareja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii (yaratanzania), ama kwa tovuti www.yara.co.tz au kwa kupiga simu bila malipo katika kituo cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750188.
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Deodath Mtei (kulia), akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya aina ya Boxer 150-UG yenye thamani ya shs milioni 3 kwa mshindi wa kampeni ya Programu ya uaminifu ya YaraConnect, Hussein Kaniki (wa tatu kushoto), mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika dukani kwake katika Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga jana.
Bwanashamba Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Novatus Salala (kushoto), Bwanashamba mwingine wa Yara, Omary Hussein (katikati), na mshindi wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Hussein Kaniki (wa pili kushoto), wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ghala la kuhifadhia mbolea la duka la mshindi huyo katika hafla ambayo Yara ilimkabidhi Bwana Kaniki pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3 ikiwa ni zawadi ya ushindi wa kampeni ya YaraConnect inayoendelea. Kulia ni Meneja Masuluhisho ya Kidigitali, Deodath Mtei na Mratibu wa Miradi ya Kidigitali, Eliwaza Mzonge.
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Deodath Mtei (kulia), akizungumza katika hafla ambayo Yara ilimkabidhi Bwana Hussein Kaniki (wa pili kushoto), mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet, pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3 ikiwa ni zawadi ya kampeni ya uaminifu ya yaraConnect katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga jana. Wengine ni wafanyakazi wa Yara.
Bwanashamba wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Omary Hussein (kulia), akizungumza katika hafla ambayo Yara ilimkabidhi Bwana Hussein Kaniki, mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet, pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3 ikiwa ni zawadi ya kampeni ya uaminifu ya yaraConnect katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga jana.
mshindi wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Bwana Hussein Kaniki, mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet, akitoa shukurani zake kwa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki mpya yenye thamani ya shs milioni 3 baada ya kuibuka mshindi wa kampeni hiyo inayoendelea. Aliwata wauzaji wenzake kujisajili na programu ya yaraConnect ili waweze kushinda zawadi kama yeye.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Lushoto, mkoani Tanga, wakimsikiliza Bwanashamba Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Novatus Salala (katikati), akizungumza kuhusu faida na matumizi sahihi ya Mbolea bora ya Yara, katika hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3, kwa mshindi wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Bwana Hussein Kaniki wa dula la Kaniki Agrovet lililopo kijijini hapo. Makabidhiano yalifanyika kijijini Manolo Jana.
No comments: