SUA YAIBUKA KIDEDE KWA TAASISI ZILIZOSHIRIKI KWENYE MAONESHO YA NANENEN KANDA YA MSHARIKI
NA FARIDA SAID, MOROGORO.
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la vyuo vikuu na vyuo vya kati kwenyemaonesho ya nanenane kanda ya mashariki yaliofanyika mkoani morogoro na wapili kwa kundi la washindi wa jumla katika kanda hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa ushindi huo Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya elimu ya kujiendeleza Prof.Dismas Mwaseba alisema wamefurahishwa na ushindi huo na wanajipanga kwa maonesho yanayofuata ili kupata ushindi kwa mara nyingine.
“Leo kwetu ni siku ya furaha kubwa kupata ushindi wa pili kwa mshindi wa jumla na ushindi wa kwanza kwa taasisi zilizoshiriki maoneosho haya, nitoe pongezi kwa watumishi wote wa SUA walioshiriki katika kuonesha teknolojia mbalimbali kwenye viwanja hivi na kiifanya SUA kuibuka kidedea.” Alisema Prof. Mwaseba
Aidha alisema wanaenda kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika maonesho ya mwaka huu ili mwaka unaofuata waweze kushika nafasi ya kwanza kwenye maonesho hayo.
Alisema ushindi huo umechagizwa na teknolojia mbalimba ambazo SUA imezionesha katika maonesho hayo ikiwemo vipandwa vya mazao mbalimbali, mifugo, mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia simu ya mkononi pamoja na ndege isiyo na rubani(Drone ) inayomsadia mkulima kukagua shamba kwa kupiga picha na kuona maendele ya shamba.
No comments: