SHULE ZA ATLAS KUWA NA MAGARI 10 SEPTEMBA SHULE ZINAPOFUNGULIWA
Wafanyakazi wa Kampuni ya Atlas Mark na wafanyakazi wa Benki ya UBA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo kwaajili ya kuboresha huduma za usafiri katika shule za Atlas jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mipango, Fedha, Utawala na Sheria wa Atlas Mark Group, Didas Kanyambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa wakisikiliza kwa makini mfanyakazi wa benki ya UBA wakati wa majadiliano ya makubaliano ya ushirikiano na shule hiyo.
Wafanayakazi wa Benki ya UBA na Shule ya Atlas wakiendelea na majadiliano mbalimbali juu ya masuala ya shule ya Atlas jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Majanga wa Benki ya UBA Afrika, Layi Sofolahan kutoka nchini Nigeria akizungumza wakati alipotembelea na kujionea miundombinu ya Shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Atlas na Benki ya UBA wakitembelea mazingira ya shule wakitembelea miundombinu ya shule ya shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam.
SHULE zinazomilikiwa kampuni ya Atlas Mark Group wakishirikiana na Benki ua UBA hapa nchini waendelea kuboresha miundombinu ya usafiri katika shule hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Agosti 18, 2022 Mkurugenzi wa Mipango, Fedha, Utawala na Sheria wa Atlas Mark Group, Didas Kanyambo amesema kuwa benki ya UBA wamesema watatoa mkopo kwa shule hiyo ndani ya wiki mbili zijazo ili kuweza kulipia magari 10.
Amesema kuwa magari hayo 10 tayari yapo bandarini yaliyokuwa yameletwa na Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd kutoka nchini Japani.
"Shule zinapofunguliwa mwezi wa Tisa tarehe 5 tutakuwa tayari na mabasi 10 ili kuboresha huduma ya usafirishaji katika shule za Atlas, tutakuwa na usafiri ambao umekamilika kwani benki ya UBA wameshatupa uhakika wa baada ya wiki mbili." Amesema Kanyambo.
Amesema kuwa wanahitaji kuwafikia wateja wengi zaidi na wanafunzi wafurahie huduma ya usafiri waendapo shuleni na warudipo.
Kwa upande wa Mkurugenzi mwenza wa Kampuni hiyo, Zana Rugambwa ametoa wito kwa wazazi walezi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo kwani wamejizatiti katika kuimarisha huduma zao hasa za usafiri kwa wanafunzi wa kutwa na mabweni kwa wanafunzi wa bweni.
"Ni ndoto zetu kutoa huduma bora kwahiyo wadau wote muwe na imani na kutoa ushirikiano na Atlas UBA sasa yanaaza kuonekana, baada ya wiki mbili tutakuwa tumeshayaleta magari 10 katika shule zetu ili kuwarahisishia usafiri watoto watokapo nyumbani na kurudi nyumbani." Amesema Zana
Amesema magari hayo 10 yataanza kufanya kazi punde tu shule zitakapofunguliwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa amesema kuwa kukamilika kwa ununuaji magari hayo kutaboresha suala la usafiri katika shule hizo.
Kuanzia mwaka huu hadi Juni 2023 tunatarajia kuwa tumeingiza mabasi Mapya 40 na ambayo yametumika kwa miaka michache na mpaka sasa tunavyoongea 10 yapo bandarini."Amesema Rugambwa
Kwa upande wa Meneja wa Fedha shule za Atlas, Anna Lupembe amesema kuwaujio wa wafanyakazi wa benki ya UBA umeonesha mwanga kwa Atlas kwani sasa matarajio yao yatakamilika baada ya wiki mbili.
Mkuu wa wateja wakubwa,wadogo na wa kati wa Benki ya UBA, Peter Temu amesema ushirikiano wao na Shule za Atlas unamanufaa makubwa kwa jamii, benki ya UBA wanaweza kutatua changamoto yao.
"Tunaweza kutatua changamoto yao kwa haraka, kwa wakati kabla shule hazijafunguliwa." Amesema Temu
Mkuu wa Matawi ya Benki ya UBA, Mwinyimkuu Ngalima amesema kuwa Atlas ni mdau Mkubwa wa shule hizo kwahiyo Atlas na UBA tutaendelea kusukuma Gurudumu la maendeleo ili iwe mfano kwa shule nyingine.
Amesema UBA wanampango maalumu kwenye shule mbalimbali ambazo zinataka fedha kutoka benki hiyo katika maendeleo ya Shule.
No comments: