SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA KAMPUNI YA UNILEVER



Pichani kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja kwa pamoja wakizindua muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dodoma.

 

 MKUU wa Mkoa wa Dodoma My Rosemary Senyamule ameipongeza Kampuni ya Unilever ambayo ni watengenezaji wa Sabuni ya Omo kwa namna ambavyo wamekua mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika mambo ya kijamii.


Mh. Senyamule ametoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi ambapo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.

Mh. Senyamule amesema Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Omo wamekua wadau wakubwa wa Serikali na Watanzania kwa ujumla na kwamba anafarijika kuona wakizindua muonekano mpya wa Sabuni hiyo.

" Wote tunatambua ya kwamba Unilever ni kampuni kubwa na ya kimataifa ambayo bidhaa zake wengi wetu humu hutumia kila siku. Kuna sabuni ambazo kila siku tunatumia kwenye kufua, mafuta ambayo kila siku tunajipaka na royco ambayo ukitaka mboga iwe tamu lazima tutumie.

Bidhaa za Unilever ni bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na zimekidhi vigezo vyote vya kimataifa. Ninayo furaha kushiriki kwenye uzinduzi huu wa muonekano mpya wa sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi," Amesema Mh Senyamule

Amesema Unilever Tanzania na Sabuni yao ya Omo wamekuwa Mstari wa Mbele katika kushiriki mambo ya Kijamii katika mkoa wetu wa Dar es salaam hususani katika kutoa Msaada wa Shuka Pamoja na sabuni kwenye Hospital za Muhimbili Hospitali, Mwananyamala Hospitali na Amana Hospitali zilizopo jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Ninja amemshukuru Katibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam,Mkuu wa mkoa wa Dodoma na serikali kiujumla kwa kufika kushiriki tukio hilo la uzinduzi wa muonekano mpya wa Sabuni ya Omo ambapo pia amewahakikishia watanzania kwamba ubora wa bidhaa hiyo umeongezeka maradufu.

" Kampuni ya Unilever imekuwa ikienda sambamba na ukuaji wa teknolojia duniani ili kuendana na hali ya soko na hususani kwa wateja wake.

 
hivyo leo ni siku muhimu sana kwetu kwani tunazindua muonekano mpya wa sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi kwa lengo la kuendelea kuvutia watumiaji wa sabuni hii.

Naomba nichukue fursa hii kuwaambia wateja wetu na jamii ya Kitanzania kwamba ujumbe wetu kwa leo ni kuwa OMO NI MKALI WA MADOA SUGU ni sabuni namba moja kwa kuondoa madoa sugu na kwa haraka zaidi kwani unga na vimeng’enya viliyomo ndani mwake ni mzuri na huondoa uchafu kwa haraka Zaidi na kuacha nguo yako ikiwa na harufu nzuri (manukato) ndani ya siku 14," Amesema Minja.

Amesema Kampuni ya Unilever kwa kupitia sabuni yake ya Omo imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kile kidogo tupatacho kwa watanzania na kuungana na watanzania katika kujenga Maisha bora kwa wote.

" Tumekuwa na kampeni mbalimbali kama MKONO WA SHUKRANI, kwa mwaka jana, kampeni hii ilifanyika katika Hospitali tatu jijini Dar es salaam Muhimbili, Mwananyamala Pamoja na Hospitali ya Amana, ambapo tulichangia mashuka Pamoja na sabuni kwa ajili ya watanzania wenzetu, Pia Omo tumekuwa na kampeni ya Mkono Wa Ukarimu, kampeni maalum kabisa wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kampeni hii ilifanyika na tulikusanya nguo kutoka kwa watanzania wenzetu na tukafua kwa kutumia Omo na pia tukaenda kuzikabidhi kwa wale watu wenye uhitaji," Amesema.










 


 

 

No comments: