MWAIKIMBA ASIMULIA JINSI ALIVYOPATA SH.MILIONI 58 ZA M-BET TANZANIA

 



Mkazi wa mkoa wa Mbeya, Ojilloh Gadson Mwaikimba akipozi na mfano wa hundi yenye thamani ya Sh58, 650,180 baada ya kubashiri kwa usahihi matokea ya mechi 12 ya ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya kampuni ya M-BET –Tanzania.

………………………….

Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam.
Mkazi wa mkoa wa Mbeya, Ojilloh Gadson Mwaikimba ameshinda kiasi cha Sh58, 650,180 baada ya kubashiri kwa usahihi matokea ya mechi 12 ya ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya kampuni ya M-BET –Tanzania.

Mwaikimba ambaye ni shabiki wa timu ya Manchester City alisema kuwa haikuwa rahisi kushinda fedha hizo kutokana na ugumu wa kubashiri mechi mbalimbali na hasa kipindi ambacho ligi zilikuwa zimesimama huku timu chache zikienda kufanya mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu (Pre-season).

Alisema pamoja na changamoto hiyo, Mwaikimba ambaye ni mwalimu kitaaluma, aliweza kufanya ubashiri wake kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kupata fedha hizo.

Alifafanua kuwa alishinda fedha hizo wiki kadhaa zilizopita, lakini kutokana na tatizo la usajili wa simu yake hakuweza kupata fedha hizo katika muda huo kutokana na utaratibu wa kampuni ya M-BET.

Alifafanua kuwa alisajili laini yake ya simu kwa kutumia kitambulisho cha Taifa cha mtu mwingine, hali ambayo ilimfanya kuchelewa kupata fedha hizo.

“Jina langu halisi na lile usajili lilikuwa tofauti na hivyo M-BET kushindwa kunilipa fedha kwani ingekuwa ni kinyume na taratibu. Ilinilazimu kuanza kufuata utaratibu wa usajili kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano na taratibu za M-BET na kulipwa fedha zangu.

Nimeamini kuwa hali ya mtu haipotei kwani baada ya kushindwa kulipwa mara ya kwanza na kupewa utaratibu, nikawa na mawazo mengi sana kuhusiana na fedha hizo. Naishukuru M-BET Tanzania kwa kunikumbusha kuhusiana na kufuata taratibu za usajili wa laini za simu kwa majina sahihi na pia ninatoa wito kwa waliojisajili kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine, wafuate utaratibu,” alisema Mwaikimba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wataendelea kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na taratibu na kuwaomba watu wenye usajili tofauti na kitambulisho cha Taifa kufanya marekebisho.

“Nampongeza Mwaikimba kwa ushindi huu mnono ambao utamwezesha kuwa miongoni mwa washindi wetu ndani ya nyumba ya mabingwa, Pia nawakumbusha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa la Taifa,” alisema Mushi.

No comments: