MILLARD AYO TV WAPEWA ONYO, WAASWA KUWAOMBA RADHI MARA TATU WATAZAMAJI WAKE
Mwenyekiti kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Habbi Gunze akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2022. wakati wa kuwasilisha uamuzi wa kamati ya Maudhui kuhusu mashtaka ya ukiukwaji wa kanuni za mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni), 2022.
Mwenyekiti kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Habbi Gunze akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2022. wakati wa kuwasilisha uamuzi wa kamati ya Maudhui kuhusu mashtaka ya ukiukwaji wa kanuni za mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni), 2022.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) imekitaka kituo cha Televisheni ya Mtandaoni cha Millard Ayo kuwa na bodi ya uhariri inayoundwa na wataalamu wa Uandishi wa Habari ili kuwasaidia katika kufanya Uchambuzi na maamuzi Sahihi yanayozingatia taaluma katika kazi zao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Habbi Gunze wakati akiwasilisha uamuzi wa kamati ya Maudhui kuhusu mashtaka ya ukiukwaji wa kanuni za mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni), 2022 kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 9, 2022. Amesema kuwa chombo hicho kihakikishe kinadumisha utamaduni wa kitanzania wa kuheshimu, kutunza na kulinda utu wa binadamu pamoja na heshima ya marehemu katika kuwasilisha maudhui ya habari.
Gunze akiwakilisha kamati ya Maudhui hiyo amesema kuwa ni kosa kisheria kupiga picha na kuonesha au kusambaza kwenye mitandano ya kijamii miili ya watu waliofariki dunia kwa ajali au namna yeyote ile.
Gunze ametahadhalisha vyombo vya habari na mitandao ya kijamii itakayochapisha na kusambaza picha za marehemu kwa namna yeyote ile kuwa itachukuliwa sheria kali dhidi ya wanaohusika.
Kufuatia Millard Ayo Televisheni TCRA kupitia Kamati ya Maudhui imejiridhisha kuwa imekiuka kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni) ya 2020.
Millard Ayo Televisheni imepewa onyo na imeamriwa kuomba radhi kwa watanzania wake mara tatu kwa Siku tatu Mfululizo kupitia chombo chake kilichotumika kutenda kosa.
Awali Gunze amesema kuwa Millard Ayo Televisheni Julai 26, 2022 ilirusha na kuonesha picha za kutisha za miili ya watoto wa shule ya Msingi ya King David waliofariki dunia katika ajali ya basi la shule iliyotokea eneo la Mjimwema nje kidogo ya mji wa Mtwara.
Amesema kuwa Millard Ayo Televisheni kwa kurusha na kusambaza Picha hizo ilikiuka kanuni za maudhui ya Mtandaoni namba 9 (a) 12 (a) 16 (1 na 2) pamoja na aya ya 3 (i) ya jedwali la tatu katika kanuni za mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (Maudhui Mitandaoni) 2020.
Licha ya hayo wakati wa kuwasilisha Utetezi wa Maandishi, Mkurugenzi Mtendaji wa Millard Ayo Televisheni, Millard Ayo, alikiri kuchapisha maudhui hayo anayotuhumiwa nayo na walikili kuwa ilikuwa ni bahatimbaya licha ya Mwandishi alijisahau kupandisha mtandaoni Cover ambayo haikutakiwa kwenda.
Waliendelea kudai kuwa Mwandishi alikuwa anafahamu kwamba kuchapisha picha za Marehemu ni Kinyume cha kanuni na maadili ya uandishi wa habari ndio maana picha hizo zilifutwa ndani ya muda mchache baada ya kupandishwa mtandaoni.
No comments: