KIONGOZI WA TAKUKURU DODOMA AIPONGEZA TTCL KWA MABADILIKO
Afisa Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Geophrey Mlewa akiwapa maelezo wanafunzi wa Falsafa na Maadili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao wapo katika mafunzo ya vitendo (Field) katika Ofisi ya Taasisi ya TAKUKURU Dodoma, kuhusu huduma zinazotolewa na Kituo cha Taifa cha kuhifadhi Data Kitandao (NIDC) walipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika ngazi ya Kanda katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Afisa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Frank Tibelelwa (kushoto) akiwapa maelezo wanafunzi wa Falsafa na Maadili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao wapo katika mafunzo ya vitendo (Field) katika Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania Dodoma, kuhusu huduma ya Faiba Mlangoni inavyofanya kazi walipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika ngazi ya Kanda katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Afisa Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Robert Lwamahe (kushoto) akiwapa ufahamu wanafunzi wa Falsafa na Maadili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao wapo katika mafunzo ya vitendo (Field) katika Taasisi ya TAKUKURU Dodoma, juu ya huduma zitolewazo na Kitengo cha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na mikongo ya Baharini ya Seacom na Easy OFC inayoungana na Mkongo wa Taifa, walipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika ngazi ya Kanda katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JAMII imeaswa kuzingatia suala la maadili kuweza kuzalisha watu watakao kuwa na uzalendo na nchi yao katika kulinda, kutunza rasilimali za Taifa ikiwemo miundombinu ya mawasiliano ambayo ndiyo kiungo muhimu katika nyanja ya usalama.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mkufunzi Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Dodoma, Bw. Faustine Malecha alipotembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania, TTCL katika maonesho ya Siku Kuu ya Wakulima yanayofanyika Kanda ya Kati kwenye Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Bw. Malecha aliyeambatana na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaosomea Falsafa na Maadili walioko katika mafunzo ya vitendo TAKUKURU Dodoma, ameipongeza TTCL kwa hatua kubwa iliochukua kuhakikisha inarejesha huduma bora za mawasiliano kwa Watanzania.
Amesema mtazamo aliokuwa nao kuhusu TTCL na baada ya kufika bandani hapo na kupokelewa vizuri na moafisa waliotumia utaalam wao kuelezea shughuli kubwa zinazofanywa na shirika hilo, amebaini kuwa kuna mabadiliko makubwa kimaendeleo ikilinganishwa na lilivyokuwa hapo awali.
Amesema TTCL ni mpya ambayo kwa sasa imejipambanua kutoa huduma za kisasa kulingana na maendeleo ya teknolojia, mbapo sasa inatoa huduma bora kwa haraka huku ikiwezeshwa na faiba inayotoa huduma za mawasiliano kwa viwango vya juu.
“nimefurahishwa sana na jinsi huduma zilivyopanuka kutoka zilivyokuwa maana sasa TTCL inasikika na huduma zinawafikia watu wengi zaidi,” alisema Malecha.
Akizungumzia suala la uadilifu Bw. Malecha amesema TTCL ni chombo muhimu kinachotegemewa na Serikali ndio maana kimeaminiwa na kupewa jukumu la kusimamia miundombinu ya mawasiliano ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) pamoja na Kituo cha Kutunza kumbukumbu (NIDC).
Amewashauri watendaji wa shirika hilo kutoiangusha Serikali na hivyo kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa kuzingatia weledi, uadilifu na uzalendo kwa taifa, huku wakizingatia kuwa chombo hicho wanachokisimamia ni muhimu sana katika kulinda usalama wa taifa lao.
Alisema ni wazi kuwa teknolojia ya kuwafikishia wateja huduma yamawasiliano kwa njia ya faiba mpaka majumbani na ofisini ni huduma inayohitaji watumishi waadilifu na wanaojituma na kulipongeza shirika hilo kuwa na watu wa aina hiyo ambao wamewezesha huduma hiyo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioambatana na Bw. Malecha bandani hapo, wamewaongeza watoa huduma kwa mapokezi yao na kuweza kuwaeleza shughuli na majukumu ya TTCL kwa wananchi na Taifa kwa ujumla jambo ambalo limewajenga kiuelewa.
Hata hivyo wananfunzi hao wamelishauri shirika hilo kuto subiri maonesho ya kitaifa kutoa elimu kwa jamii bali, kwenda mbali zaidi kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha elimu kuhusu TTCL inawafikia wananchi wengi zaidi.
“Inaonekana TTCL inajukumu zito kwa Taifa letu lakini si watu wengi wanalifahamu hilo, na hata hapa kwenye maonesho wengi wananshindwa kuingia kutokana na kukosa kiingilio hivyo nivizuri litumie njia mbadala ili kuwafikia watu wengi zaidi,” Alisema Liberatus mmoja wa wanafunzi hao. Maadhimisho ya Siku Kuu ya Wakulima huadhimishwa kila Agosti 8 ya kila mwaka ambapo hutanguliwa na maoenesho ya shughuli mbalimbali zinazohusu wakulima, Wavuvi na Wafugaji huku Wizara, Taasisi, Mashirika ya Serikali na yasio ya kiserikali hushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo lengo likiwa ni kuwafikia wadau na kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa kazi za serikali kupitia taasisi hizo.
Afisa Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Doreen Moshi akimwelezea Afisa Mkufunzi Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya TAKUKURU Dodoma, Bw. Faustine Malecha umuhimu wa kuwa na kadi ya N-Card katika matumizi mbalimbali ya fedha mtandao zinazotolewa na Kituo cha Taifa cha kuhifadhi Data Kitandao (NIDC) walipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika ngazi ya Kanda katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
No comments: