KATIBU MKUU CCM ASEMA WILAYA YA MUHEZA KUNA SHIDA YA UONGOZI, AACHIA UJUMBE MZITO…


 Na Mwandisi Wetu, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameonesha kusikitishwa na namna ambavyo viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga wamekosa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Kutokana na hali hiyo Chongolo ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho pamoja na kuzungumza na Wana CCM amesema hafurahishwi hata kidogo na hali aliyoiona kwenye Wilaya hiyo na hivyo kuwataka viongozi kuheshimiana na kutekeleza majukumu yao ambayo wamepewa.

“Mimi napita huku kwa ajili ya kujiridhisha , kufanya ukaguzi kuona kwa macho na  kusikiliza wanaotegemea ili nikitoka niwe na amani lakini hapa  kuna shida ya uongozi , mimi ni Katibu Mkuu wa CCM yenye Serikali,siwezi kuondoka nisiseme na  hata nikiondoka tutafuatilia .

“Niwe mkweli hapa Muheza mambo hayawezi kwenda kwa kasi tunayotegemea katika mazingira kama haya, nimetoka Lushoto  jana unaona ushirikiano , unamuona kila mmoja anajua anachokifanya.Hapa hakuna , hapa hakuna, hapa hakuna.

“Inaonesha kila ofisi ni ya…hatuwezi kwenda hivyo hata kidogo  viongozi wenye dhamana hapa nendeni mkakae mjue mmeletwa kuwatumikia wananchi sio starehe, sio mambo binafsi  na hapa Mkuu wa Wilaya aliyeletwa na serikali awe mfupi awe mrefu , awe mwembamba awe mnene ndio Mkuu wa Wilaya.

“Umeletwa hapa unajukumu la kusimamia Serikali kama kuna mtu mrefu kuliko wewe ajue wewe ndio uliopewa dhamana lakini wewe ndio unatekeleza majukumu yako , kiongozi wako ni huyo RAS awe na umri mdogo ndio kiongozi wako, kiongozi wako ni Mkuu wa Wilaya hata akiwa mdogo.

“Wakuu wa Idara lazima mjue hivyo Mbunge anamategeo makubwa yeye amekuja ameomba dhamana ya wananchi anategemea makubwa , msipofanya vizuri mnamkwamisha, madiwani wanataka matokeo , msipokaa vizuri mnawakwamisha , Chama hiki kilijinadi kikahangaika na  kikajitangaza asubuhi mchana, jioni hapa tunataka hili litokee na haya ndio tunaahidi,”amesema Chongolo.

Ameongeza wasipokaa sawasawa watashindwa kufikia malengo.“Nasema nisikilizeni tena mimi nimekuwa Mkuu wa Wilaya miaka sita , nimekuwa Mkuu wa Wilaya Longido , huyu Katibu wenu alikuwa Mwalimu wa shule ya msingi tena mwalimu mkuu…

“Akanifuata siku moja ofisini kuniambia anataka kuacha kazi nikamwambia unakichaa , mwalimu mkuu anaacha kazi awe Mwenezi ambako hana mshahara hata wa shilingi moja , nilivyokuwa Katibu Mkuu nikasema ngoja nimpe kazi kwasababu anakipenda Chama chake.”




No comments: