PHOENIX ASSURANCE YAZINDUA BIMA MAALUM KWA WASAFIRISHAJI,BIMAPLUS

 


Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam.

Kampuni ya Bima ya Phoenix Assurance imezindua huduma ya BimaPlus kwa wamiliki wa magari makubwa ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

BimaPlus itawawezesha wafanya biashara hao kulipwa fidia ya bidhaa zao na gari husika endapo watapatwa na majanga mbalimbali (ajali) wakiwa njiani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Phoenix Assurance Bw Ashraf Musbally alisema kuwa lengo kubwa la huduma hiyo ni kulinda mtaji wa mfanyabiashara kwa wateja wao watakao jiunga na bima kubwa au Comprehensive.

Bw. Musbally alisema kuwa wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zinazokwenda mikoani au nje ya nchi wanakuwa na wakati mgumu wa mali zao kufika salama kutokana na matatizo mbalimbali ikiwa pamoja na wizi.

Alisema kuwa kupitia BimaPlus, mfanya biashara atakuwa na uhakika wa mali zake ikiwa pamoja na chombo cha usafirishaji.

“Kupitia BimaPlus, msafirishaji atakuwa na uhakika wa mali na mtaji wake kwani kampuni yetu itakuwa tayari kulipa fidia endapo kutatokea mali husika kupotea,” alisema Bw Musbally.

Alisema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa wafanyabiashara na kuwaomba kujiunga nayo kwani inalpa fidia kwa dereva, utingo, mmliki wa mzigo na mjanga ikiwa mke au mume wa mnufaika ambao watafidiwa kiasi cha sh mlioni 2.

“Uanzishwaji wa huduma ya BimaPlus ni muendelezo wa ubunifu na upanuaji wa shughuli zetu katika soko la bima hapa nchini. Lengo letu ni kumfaidisha mteja wetu na kuwa na amani katika shughuli zake. Kupitia kwa BimaPlus, mteja wetu atakuwa na uhakika wa biashara yake kwa sababu mali (bidhaa) zitakuwa salama na vilevile chombo cha usafirishaji. Kampuni yetu italipa fidia kwa majanga yoyote yatakayotokea,”alisema Bw.Musbally alisema kuwa huduma ya BimaPlus pia inamlipa fidia dereva na wafanyakazi wengine katika gari husika ebdapo watakuwa wamepata ajali.

Alisema kuwa pia BimaPlus inalipa fidia nyingi endapo muhusika atapata wakati wa usafirishaji wa bidhaa husika na vile vile italipa fidia ya gharama za usalama au ulinzi. Alisema kuwa kampuni yao imejipanga kuendeleza huduma ya bima nchini na ndiyo maana wamekuwa wabunifu kwa lengo la kumnufaisha mteja.

“Phoenix imekuwa mwanzilishi wa ubunifu wa bidhaa zilizopo kwani ilikuwa ya kwanza kuja na ubunifu kama vile huduma ya Usaidizi wa Barabara ambayo ni utulivu.

Alisema ili kutoa huduma za haraka, wameanzisha kitengo cha huduma ambacho kinafanyakazi masaa 24 na watakuwa wanalipa fidia kwa muda usiozidi siku 30.

Kwa upande wake, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA), Bw Frank Fred aliipongeza kampuni ya Phoenix Assurance kwa kuanzisha bima hiyo ambayo inaleta suluhisho kwa wafanyabiashara wasafirishaji nchini.

Bw Fred alisema kuwa bima hiyo inawapa uhakika wafanyabiashara wa sekta ambayo imekuwa na changamoto kadhaa.

Alisema kuwa bima hii ya BimaPlus itachangia katika kujenga uchumi nchini na TIRA itaendelea kuunga mkono jitahada na ubunifu wa Phoenix Assurance katika kuleta maendeleo nchini.

Wakati huo huo; Kamanda Msaidizi wa Usalama barabarani hapa nchnim Kamishna msadizi wa Polisi ACP Meloe Buzema alisema kuwa bima hiyo inaleta chachu ya maendeleo ya sekta hyo hapa nchini.

“Nawapongeza kampuni ya Phoenix kwa kuanzisha bima hiyoambayo inaleta faraja kwa wafanyabiashara wa usafirishaji na kuwajali madereva pia,” alisema ACP Buzema.


Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Phoenix Assurance Bw. Ashraf Musbally (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya BimaPlus yenye lengo kubwa la kulinda mtaji wa wafanyabiashara wa usafirishaji mizigo.


Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA), Bw Frank Fred akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya BimaPlus yenye lengo kubwa la kulinda mtaji wa wafanyabiashara wa usafirishaji mizigo.


Kamanda Msaidizi wa Usalama barabarani hapa nchini Kamishna msadizi wa Polisi ACP Meloe Buzema akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya BimaPlus yenye lengo kubwa la kulinda mtaji wa wafanyabiashara wa usafirishaji mizigo.



Meneja Mkuu wa kampuni ya bima ya Phoenix Assurance Bw. Robert Kalegeya akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya BimaPlus yenye lengo kubwa la kulinda mtaji wa wafanyabiashara wa usafirishaji mizigo.
 

No comments: