Vodacom Tanzania Yakabidhi Gari Jipya la Tusua Mapene Ikiwa Sehemu ya Msimu wa Upendo


Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini, Mhe. Abbas  Kayanda (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mshindi wa gari jipya aina ya Suzuki S Presso kutoka promosheni ya Vodacom Tusua Mapene, Shemmy Chisumo funguo za gari baada ya kuibuka mshindi wa gari la kwanza la promosheni hiyo, hafla hii imefanyika kwenye viwanja vya Manyema, Mbuyuni wilayani humo. Sambamba na zawadi hiyo washindi sita walijishindia Tv za kisasa, na wengine kumi walijishindia Simujanja kutoka promosheni ya "Show Love, Tule Shangwe" zinazotolewa msimu huu wa sikukuu kwa wapendanao, ili ushinde  mteja unatakiwa kununua bando na kutumia huduma ya M-pesa, kushoto kwa mshindi ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania George Venanty aliyemwakilisha mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo.


 

Washindi wa zawadi za promosheni ya "Show Love,Tule Shangwe" wakiwa na zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Manyema Mbuyuni wilayani Moshi, jumla ya Tv sita za kisasa na simu janja kumi zilitolewa kwa wapendanao huku pia washindi wa pesa taslimu nao walikabidhiwa pesa walizoshida. Ili ushinde  mteja unatakiwa kununua bando na kutumia huduma ya M-pesa kwa kupiga *149*01#


No comments: