TANZANIA WENYEJI FAINALI ZA DUNIA MISS AFRICA GOLDEN 2022

 




Baada ya kuwa wenyeji kwa mafanikio wa fainali za dunia za Miss Tourism Worlds 2006, kupitia Miss Touirism Tanzania Beauty Pageant LTD kampuni tanzu ya Africa Tourism Promotion Centre ,Tanzania imepewa tena heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Africa Golden 2021/2022. Fainali za dunia za Miss Africa Golden 2021 / 2022,  zitashirikisha zaidi ya warembo hamsini (50) wenye mataji ya kitaifa kutoka zaidi ya nchi hamsini duniani kote.

Tarehe kamili ya kufanyika kwa fainali hizo ,itatangazwa na Rais wa dunia wa shindano hilo SAPPHIRE ADAOBI OBI katika mkutano wa kimataifa na waandishi wa habari utakao fanyika mapema mwezi Februali , 2022 jijini Dar Es Salaam, baada ya kukamilisha taratibu  na kanuni za kiserikali na mamlaka zake. Hata hivyo inatatarjiwa fainali hizo kufanyika kati ya mwishoni mwa Februali na Machi 2022.

Miss Africa Golden World, ni shindano kubwa zaidi duniani la urembo, linaloshirikisha warembo kutoka nchi zote duniani wenye asili ya kiafrika, huku fainali za mwaka huu zikiwa ni za nne tangu kuanzishwa kwake.

Tayali nchi zaidi ya arobaini (40) zimethibitisha kushiriki fainali hizo za dunia , ambazo zitafuatiliwa katika mabara yote duniani kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kielekroniki ,machapisho na mitandao ya kijamii, lakini pia kuangaliwa mbashara duniani kote kutokea katika viini vya vivutio vya utalii ,uwekezaji na utamaduni vya Tanzania bara na Zanzibar kupitia matangazo ya Televisheni na mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa nchi zilizo thibitisha kuja Tanzania kushiriki fainali hizo ni pamoja na :

Austria, Cameroon, Nigeria, Nigeria, Ghana, Sudan, Nigeria, Swaziland, Colombia, Turkey, Ethiopia, Somalia, South Sudan, Mauritius, Ghana, Rwanda, Benin Republic , Zambia, Haiti, Uganda, Dominican Republic, Nigeria, Australia, Uganda, Zimbabwe, Botswana, Namibia, Haiti, Cameroon, Mozambique, Sierra Leone, South Africa, Gambia, Austria, Benin, Burundi, Guinea, Kenya, Canada, France, Germany, India, Montenegro, Angola, Japan, Russia, United Kingdom, Malawi, United State of America, Greece, Spain, Tanzania  etc

Wakiwa nchini,washiriki wakiambatana na waandishi wa habari za televisheni, redio, magazeti ,mitandao ya kijamii, wapiga picha za video na minato , watafanya ziara za promosheni katika vivutio vya utalii,utamduni,huduma za misitu, hifadhi za bahari, wanyama pori, mazingira, uwekezaji, maliasili nyingine za taifa na meneo ya vipaumbele vya serikali na wadhamini wakipiga picha za matangazo, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii , huku wakitangaza na kuhamasisha utalii, utamduni, uwekezaji, uhifadhi, maendeleo ya kijamii na kiuchumi mijini na vijijini.


Hii ni fulsa nyingine kwa Tanzania kujitangaza kitaifa na kimataifa, huku wakihuisha, kujipenyeza na kuendeleza masoko ya kitaifa na kimataifa ya bidhaa,huduma na uwekezaji.

Tunaishukuru bodi ya dunia ya Miss Africa Golden World kwa kuipa heshima Tanzania miongoni mwa nchi nyingine duniani, lakini tunawashukuru pia kwa kuthamini mafanikio, mchango na ushiriki wetu katika uongozi na kamati mbalimbali za mashindano na matamasha ya dunia na kimataifa ya mashindano ya urembo na mitindo ya dunia na mengineyo ya kimataifa,hivyo kutoa fulsa kwa nchi yetu Tanzania kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za dunia za mashindano ya urembo na mitindo,likiwemo hili la Miss Africa Golden 2021/2022, Miss University World 2022-2024,Miss Tourism World 2023/2024, Miss Tourism Africa 2023,Miss Heritage World 2022/2024 n.k

Nina kuhakikishia ushirikiano bora daima,

Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa-  Utalii ni Maisha Utamaduni ni Uhai ;

Ewe Mtanzania Tembelea na Tangaza Utalii wa Tanzania.

Pamoja na Taarifa hii kwa vyombo vya habari,hapa nafungasha baadhi ya wshindi wa dunia wa Miss Africa Golden 2020/2021, baadhi ya watakao shiriki fainali wa mwaka huu,2021/2022.

Leave a Comment

No comments: