JIMBO LA KITETO,TUMETENGEWA FEDHA, TUTAZISIMAMIA KWA MACHO MAWILI-OLE LEKAITA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kiteto (Jimbo la Kiteto ) imetengewa Fedha za Utekekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya UVIKO -19 kwa ajili ya

1. Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 44 shule za Sekondari. ( Milioni 880,000,000) Tunaenda kufuta upungufu wa Madarasa ya Shule za Sekondari zote Wilaya ya Kiteto.

2. Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shikizi 57. ( Billioni. 1,140,000,000) . Kwa ajili ya maandalizi ya Wanafunzi wa Elimu Msingi.

3. Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Afya. ( Milioni 90,000,000).

4. Digital XRAY ( XRAY ya Kisasa) ( Milioni 420,000,000).

5. Gari la Wagonjwa (Ambulance)

6. Gari la Usimamizi wa Huduma za Afya.

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kugusa maisha yetu Wana Kiteto kwa kuboresha Sekta ya Afya na Sekta ya Elimu kwa kiwango cha juu.

Ahadi yetu kwa Mhe. Rais ni kuzisimamia Fedha tulizotengewa zitoe matokeo makubwa kwa ufanisi na tija.

Mungu Ibariki Kiteto

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Edward Ole Lekaita Kisau, (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

No comments: