UNLEASHED AFRIKA YAANDAA PROGRAMU MAALUM YA KUWAINUA WANAWAKE WAJASILIAMALI JAMII NCHINI
Na Mwandishi Wetu,Michuzi Blog
Kampuni ya Unleashed Afrika imeandaa programu maalum inayoitwa UWEZO Tanzania 2021 kwa ajili ya kuwainua wanawake wajasiliamali Jamii, ikiwa ni mkakati maalum wa kuwainua katika shughuli zao za ujasiliamali.
Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe amesema wao pamoja na mambo mengine wamejikita katika maendeleo ya vijana ,kukuza ubunifu ,kutafuta mbinu tofauti za kuongeza kazi kwa vijana wameona haja ya kuandaa mafunzo kwa wajasiliamali hao wanawake.
"Tunafanya kazi nyingi katika eneo hili hasa kwa kumuwezesha mtoto wa kike, tumejikita katika kukuza ujasiliamali jamii, ili waweze kutatua matatizo kwenye jamii zao, kitu ambacho tunafahamu watoto wa kike wajasiliamali wanachangamoto za kipekee , na tumefanya programu tofauti tofauti kama Tujenge TZ ,sasa hivi tuna mchakato mwingine unaitwa Nipe Dili.
"Lakini tumekuja kuona wajasiliamali jamii hasa wajasiliamali wa kike wana changamoto za kipekee na kama tunataka kuwasaidia kutatua hizo changamoto inabidi kufikiria kwa upana zaidi ni jinsi gani tunaweza kutengeneza programu ambazo zimejikita kutatua hizo changamoto, wakati kwa upande wa pili tunawafundisha jinsi ya kukuza ujasiliamali jamii zao,"amesema Mbowe.
Ameongeza anaposema rasilimali jamii zao anamaanisha biashara wanazozifanya kwa namna moja au nyingine zinanyanyuka na zinaleta manufaa kwa jamii.Programu hiyo imeanza mwaka huu na kwamba Uwezo Tanzania 2021 wamekuwa na ubia na taasisi ya Kifaransa iitwayo FollowHer." Tumekuja pamoja tumeleta Uwezo Tanzania na huu ni mwaka wa kwanza."
Ameongeza kwamba walianza kufungua usajili wa mafunzo hayo kwa watoto wa kike wakaweza kuomba , hivyo wameanza huo mchakato wa kupokea maaombi Februari mwaka huu na mchakato wa kutengeneza programu umeanza muda mrefu."Vitu ambavyo tulikuwa tunajiuliza ni vitu gani ambavyo tuviweke ,kuwe na programu ya aina gani ,
"Tumetumia mawazo mengi sana, tumetumia tafiti nyingi kuweza kuja kutengeneza kitu kama Uwezo, hivyo kuanzia Februari,Machi,Aprili watu walikuwa wanajiandikisha ,na Aprili na Mei tulikuwa na watalaam walioomba kutembelea biashara zao ili kuchagua hawa wajasiliamali wa kile ambao wamepatikana, wapo 15, Julai wamepatiwa mafunzo mazito kidogo katika ujasiliamali jamii.
"Baada ya hapo tukawakutanisha na wakufunzi kwa wiki nne na kila mtu tumemkutanisha na mkufunzi wake ili wawasaidie kutumia yale mafunzo waliyoyapata darasani ,kwasababu wakati mwingine unaweza kuwa darasani ukafurahia yale mafunzo lakini ukifika kazini haviingiliani ,kwa hiyo ikawa ni muhimu kuwakutanisha na watu ambao watawezesha yale mafunzo kuyaishi katika biashara zao,"amesema.
Amesema bada ya hapo wakawa na wiki ya mwisho ya mafunzo ambayo ndio hii ya sasa ambapo wamewakumbusha waliyojifunza na pia wamepanga michakato na mipango kazi ya miezi sita ijayo."Siyo tunamaliza programu halafu tunaagana, je baada ya miezi sita utakuwa umekuza vipi biashara yako?
"Tunakuunganisha na nani? Halafu leo tumekuwa na shughuli hii ya kuwakutanisha na wadau wengine kwenye sekta ya ujasiliamali jamii tanzania, kwanini ili kuhakikisha hawa wajasiliamali jamii wa kike hawaondoki tu na mafunzo ,bali wanaondoka na 'Conection' kama tunavyofahamu kitu kinachomtofautisha ujasiliamali na kukua kwa kasi na yule anayebaki pale pale ni 'conection' na nani anaweza kukufungulia mlango gani.
"Kukupa mawaidha gani maana tunasema watu wanaokuzunguka ndio watakaoweza kukunyanyua ,labda kule walipo kuna watu wengi wanawazunguka lakini hawana mawazo mapya kwa hiyo tumetaka kuwakutanisha na watu ambao wanaweza kuwapanua zaidi kiakili,"amesema Mbowe.
Amefafanua ndio maana wamefanya hivyo na baada ya leo kutakuwa na mchakato wa miezi mitatu kuanzia Septemba,Oktoba na Novemba na katikati ya Desemba watakuwa wanawakutanisha na watu wengine ambao wataenda kuwasaidia kule kwenye biashara ili ili kuziimarisha,
"Kwa yule anayependa kujiunga na UWEZO, huu ulikuwa mwaka wa kwanza na tunaweza kuja na huko mbele ya safari tutatoa taarifa kuhusu mipango yetu kwa miaka ijayo , kwa sasa kuna michakato inaendelea kwa wale ambao walikuwepo tumewaambia mwaka huu ulikuwa uthubutu , kuonekana,tulikuwa hatuna wafadhili ,hivyo tumejitolea kwa nguvu na damu jingi kuhakikisha tunafanya hiki kitu na sasa kimeonekana ,
"Sasa tunatafuta wadau kama umeguswa gonga mlango njoo utusaidie ,mwaka huu tumefanya Zanzibar, Kisarawe na Dar es Salaam na tunataka kufanya mikoa mingi zaidi ambayo iko nje ya Dar es Salaam, tunataka kupata wasichana wengine zaidi ,"amesema.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe akimkaribisha mdau mwenza kutoka taasisi ya FollowHer,Juliette Vigato kwa ajili ya kukabidhi vyeti vya ushiriki wa Wajasiliamali Jamii ambao walikuwa wanahitimisha mafunzo yao ya progaramu maalum ya ujasiliamali 'UWEZO TANZANIA 2021' .Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua Wajasiliamali Jamii 'UWEZO TANZANIA 2021' wakifurahia baada ya kupokea vyeti vyao vya ushiriki na kuhitimisha mafunzo yao wakiwa na Waandaaji wa Mafunzo hayo.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe akiwapongeza baadhi ya Wafanyakazi wake walioshiriki kufanikisha programu hiyo ya kuwainua Wajasiliamali Jamii.
Baadhi ya Wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua Wajasiliamali Jamii 'UWEZO TANZANIA 2021' wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti vyao vya ushiriki
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe akizungumza mbele ya wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua Wajasiliamali Jamii 'UWEZO TANZANIA' pamoja na Wadau wengine wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao na kuwaaga,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ikiendelea
Wajasiriamalia hao 'uwezo Queens' wakibadilishana mawazo na baadhi ya wadau katika suala zima la kupeana uzoefu na 'connection' katika uwanja wa Wajasiliamali Jamii
Wajasiriamalia hao 'uwezo Queens' wakibadilishana mawazo na baadhi ya wadau katika suala zima la kupeana uzoefu na 'connection'katika uwanja wa Wajasiliamali Jamii.
No comments: