TAWA YAWATAKA WALIMBWENDE MKOA WA PWANI KUWA CHACHU YA UTALII.
Na Farida Saidy, Dar Es salaam.
Walimbwende kutoka mkoa wa Pwani wamewataka watanzania kuhakikisha wanatembelea vivutio vilivyopo hapa nchini ikiwemo Pori la Akiba Pande linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) lililopo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam ili kuisaidia serikali kuongeza ukusanyaji wa mapato yake kupitia sekta ya utalii.
Wakizungumza mara baada ya kutembelea pori hilo, walimbwende hao wamesema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi hivyo katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa hapa nchini, watanzania wanatakiwa kuwa na mwamko wa kutembelea vivutio hivyo ili kujifunza na kufurahia mandhari za vitu vya asili tulivyobarikiwa.
Kufuatia Serikali kutoa fursa ya uanzishwaji wa mabaucha ya wanayamapori hapa nchi walimbwende hao walipata fursa ya kula nyamapori ya Nyati, hii ikiwa ni moja njia ya kuhakikisha wanaenda kuhamasisha wananchi kutembelea pori hilo na vivutio vingine hapa nchini.
Hata hivyo wameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa nzuri wanayoifanya ya kusimamia mapori ya akiba yaliyopo hapa nchini, hali inayopelekea kuongezeka kwa wananyama kwenye mapori hayo.
Aidha wameongeza kuwa kutokana na hali hiyo kumekuwepo na ongezeko kubwa la watalii hapa nchini kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na uhifadhi mzuri unaofanya na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Kwa Upande wake Kaimu Kamishna Msaidizi Mahusiano kwa Umma Twaha Twaibu ambaye amemwakilisha Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Nyanda amewataka walimbwende hao kuhakikisha wanalitangaza pori la Akiba la Pande ili kuwasaidia wananchi kulijua pori hilo na vivutio vilivyomo ndani ya pori hilo.
No comments: