RAS MKOA WA PWANI INJINIA HAJAT MWANASHA AHIMIZA KUKUSANYA USHURU KIBAHA MJI, MKURANGA NA CHALINZE
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Pwani(RAS) Injinia Hajat Mwanasha Tumbo amewataka viongozi wa Halmashauri tatu ambazo ni Kibaha Mji, Mkuranga na Chalinze kuzingatia misingi ya ukusanyaji ushuru ndani ya Mkoa huku akiwasisitiza Wakurugenzi kusimamia misingi ya uwajibikaji jamii .
Injinia Mwanasha amesema hayo leo alipokuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi mbalimbali za Halmashauri hizo tatu kuhusu mradi wa GIZ unaofadhiliwa na nchi za Ujerumani , Usiwis (Switzerland)na Umoja wa Ulaya.
"Tumejipanga kuwajengea uwezo kwenye mifumo ya kiufundi, utawala wa kisheria ,masuala ya fedha na tehama Ili kudhibiti mianya yote ya wakwepa ushuru" alisema Injinia (RAS) Mwanasha.
Injinia Mwanasha (RAS) aliongeza kwa kusema anatamani kuziona Halmashauri hizi tatu za Mkoa wa Pwani zikijitegemea jambo ambalo litasaidia kupunguza mzigo wa kwa serikali na kuweza kujimudu kwa kufanya mambo mbalimbali ya msingi ndani ya Halmashauri husika.
"Mapato yanaongeza usalama na amani ndani ya Halmashauri hivyo nina amini ukusanyaji wa ushuru utazingatia weledi Mkoa wa Pwani utakua mkubwa kiuchumi kwa sababu Pwani inasifika kwa kuwa na Viwanda na wawekezaji wengi, hali ya ukusanyaji ushuru kwa sasa ni zaidi ya asilimia 80 hivyo tunaamini kuwa tuna uwezo wa kukusanya ushuru kwa asilimia 100" alisema RAS Injinia Mwanasha.
Akizungumza kuhusu changamoto za ukusanyaji ushuru Mkoa wa Pwani RAS Injinia Mwanasha alisema kuwa anaonya kutokuwepo na migogoro katika kuendeleza zoezi hilo la kukusanya ushuru na kwa yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali atachukuliwa hatua Kali.
Wakati huohuo Mtaalamu Mshauri wa Mapato GIZ Raymond Nzali alisema kuwa wa Ujerumani, Uswis na Umoja wa Ulaya wako Kibaha kutengeneza mpango kazi wa shughuli ya mapato kwasababu wameona kuna haja ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
"Tumelenga zaidi katika ukusanyaji wa ushuru wa huduma, ukilinganisha ushuru wa huduma uko chini kwa asilimia 12 , kati ya biashara zote ina maana kwamba kuna wigo mpana wa mapato ambayo hayakusanywi ipasavyo" alisema Nzali.
No comments: