IBADA MAALUM KUFANYIKA KUWAENZI HAYATI BABA WA TAIFA MWL. NYERERE NA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
NA. MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameleza uwepo wa ibada na sala maalum ya kuwaombea hayati Baba ya Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi tunapoelekea kuhitimisha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2021.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mwishoni mwa wiki alipoongozana na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kwa lengo la kukagua maandalizi ya kuelekea kilele cha mbio hizo zitakazo hitimishwa katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita tarehe 14 Oktoba, 2021.
Waziri Mhagama ameeleza umuhimu wa ibada hiyo, kwa kuzingatia michango ya viongozi hao katika Taifa na kusema ni sehemu ya kuwaenzi na kuonesha heshima kwa namna walivyolitumikia Taifa.
Aliongezea kuwa, Kanisa kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi wanajukumu la kuiandaa ibada hiyo ya kipekee kulingana na heshima kubwa ya viongozi hao katika Taifa na kuonesha tunatambua michango yao kwa matendo.
“Ninatambua mchango wa kanisa katika nchi yetu, nikushukuru baba Askofu Flaviana kwa kuonesha uzalendo na utayari wa kuandaa ibada hii muhimu nitoe rai muendelee kuiombea siku hiyo na Taifa kwa ujumla ili kuduma katika Amani na Mshikano,”Mhe. Mhagama
Aliongezea kuwa, tukio hili ni muhimu kwa kuzingatia mbio za Mwenge kwa mwaka huu zimekua ni maalum kwani ni mara ya kwanza kuhitimishwa mbele ya Rais wa kwanza mwanamke nchini hivyo ni tukio la kihistoria.
“Mbio hizi ni maalum kwa kuzingatia maeneo muhimu matatu ikiwemo; Taifa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano akiwa madarakani, Taifa kuongozwa na Rais mwanamke wa kwanza na kuupa heshima mkoa wa Geita kuzingatia ni mkoa aliozaliwa na kuzikwa Rais wa Awamu ya Tano hayati Dkt. Johh Pombe Magufuli,” alisisistiza Waziri Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule alieleza Mkoa umejipanga kuhakikisha sherehe za Mbio za Mwenge zinafana na kuzingatia wamebakiza siku chache na kuahidi kuendelea kushirikirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wadau wote katika kuifikia siku hiyo.
"Mkoa utaendelea kufanya maandalizi muhimu katika ubora unaoendana na hadhi ya Mkoa wa Geita na kuzingatia heshima tuliyopewa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita,"alisema Rosemary
Naye Waziri wa Nishati Dkt.Medarn Kalemani alimshukuru Waziri Mhagama kutenga muda kutembelea na kukagua maendeleo ya maandalizi ya sherehe za kilele cha Mbio hizo nakuendelea kuwaasa wananchi wa Chato kuonesha ushirikiano wao kwa Serikali ili kufanikisha tukio hilo.
Akitoa neno la shukran Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala amesema wataendelea kuliombea Taifa na kuhubiri upendo, amani na mshikamano ili kuendelea kuwa na Taifa lenye utulivu.
“Sisi viongozi wa dini tunaungana nanyi kuifanikisha siku hiyo katika kujiandaa na ibada hiyo maalum na nitaliwasilisha katika baraza kulinga na uzito wake”Alieleza Askofu Kassala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule .wakisaliana na Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala mara baada ya kuwasili katika ofisi za kanisa hilo Septemba 04,2021 kwa lengo la kuteta kuhusu maandalizi ya Kelele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kikao na Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala katika ofisi zake Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule akieleza jambo kuhusu maandalizi ya mkoa katika kuelekea cha Sherehe za Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni walipomtembelea Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala katika ofisi za kanisa hilo Mkoani Geita.
Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala akieleza namna kanisa lilivyojipanga kuendelea kuombea Taifa alipotembelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani pamoja na Timu kutoka mkoa wa Geita ili kujadili maandalizi ya kuelekea kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021.
Akofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Flavian Kassala akiongoza maombi ya maalum ya Viongozi waliomtembeela na Serikali kwa ujumla bara baada ya kikao hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments: