DC KALISTI LAZARO ASISITIZA MAOMBI YAZIDISHWE MTIHANI DARASA LA SABA

 Raisa Said, Lushoto

Zikiwa zimebaki siku chache darasa la saba kufanya mtihani wao wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro amewaomba viongozi wa Dini na wazazi kufanya maombi ili Wanafunzi wapate ufaulu mzuri.

Wito huo umetolewa  na Mkuu huyo wa wilaya  wakati wa misa ya shukran ya  Fadher Africanus Kanju  baada ya kusimikwa kuwa Padre wa kanisa katoriki.

  Lazaro alisema  Wilaya ya Lushoto imekuwa haifanyi vizuri katika matokeo ya kila mwaka ya darasa la saba  hivyo alieleza ni muhimu viongozi wa dini wakafanya maombi ili huyo shetani anayefanya watoto wasifanye vizuri asipate nafasi kipindi hiki.

"Nimeangalia takwimu ya matokeo ya kitaifa ya darasa la saba nikakuta shule nane za mwisho zipo katika wilaya yetu ya Lushoto jamani hii ni aibu na fedheha"Alisema  Mkuu huyo wa wilaya.

Alisema kuwa Serikali  inatumia rasilimali kubwa na inatoa elimu bure inapaswa walimu wajitoe katika ufundishaji ili kupatikane  Matokeo mazuri na hatimaye kama wilaya waondokane  katika mnyororo  wa kushika mkia.

Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa katika kupambana na matokeo mazuri wameamua kuanzisha makambi katika shule zote za wilaya hiyo  lengo ni kuongeza ufaulu katika wilaya ya Lushoto kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya huyo amewataka wananchi kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa corona ili kujikinga na ugonjwa huo ambao kwasasa ni hatari .

Alisema kuna watu wanaogopa kuchanjwa chanjo ya corona lakini kwa waganga wakienyeji wanakwenda na wanachanjwa na hawaogopi.

Aliongeza  kuwa kwasasa wilaya ya lushoto ina Jumla ya vituo  18 vya kuchanjia  na magari mawili kwaajili kupeleka huduma pembezoni za wilaya hiyo.

Kwa upande wake Padre  Kanju alishukuru  kwa kupata upadrisho  na akasema kuwa  Safari yake imeanza  na kunachangamoto nyingi  hivo akaomba wamuombee.




 

No comments: