Watendaji waagizwa kutoa ushirikiano kwa MVIWATA wilayani Masasi
Na Amiri Kilagalila
Kutokana na ufanisi wa mbegu ya asili iliyoonyeshwa na shirika la MVIWATA, afisa tarafa ya Mchauru wilayani Masasi Titho Stambuli ameagiza maafisa watendaji kutoa ushirikiano kwa shirika Hilo.
Stambuli ametoa agizo hilo alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya mbegu za Asili yaliyoandaliwa na shirika hilo yaliyofanyika kiwilaya katika kata ya Mchauru kijiji cha Namombwe,
"Shirika la MVIWATA ni nguzo mhimu katika kuwainua wakulima,kuwajengea uwezo, uhifadhi wa mbegu,kuongezeka kwa uzalisha na ni watetezi wa wakulima"Alisema Stambuli
Aidha amesema ofisi yako ipo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa shirika hilo ili kuwaletea maendeleo wakulima.
"Nimeagiza watendaji kutoa ushirikiano kwa shirika na pia kwangu milango iko wazi katika kuwapa ushirikiano ili mradi mkulima anufaike na shirika"
Vile vile bwana Stambuli amesema serikali inaendelea kutatua kila aina ya Changamoto inayo mkuta mkulima ikiwemo swala la pembejeo ili kufanya kilimo chenye tija na shirika la Mviwata kuwa na tija kwa jamii kwa kupata matokeo chanya
No comments: