MELI KUBWA ILIYOBEBA VIUATILIFU TANI 2850 KWA AJI YA KUTIBU MAGOJWA YA KORSHO YATINGA MTWARA
Ni Meli kubwa ambayo Leo mapema imewasili katika Bandari ya Mtwara, Mkoani Mtwara ikiwa imebeba viuatilifu tani 2850 Kwa ajili ya kutibu magonjwa ya Korosho. Ujio wa Meli hiyo ya MV YASEMIN imetua katika Bandari ya Mtwara ikitokea nchi za Uarabuni.
Akizungumza mara baada ya Meli hiyo kuwasili, Meneja wa Bandari ya Mtwara Mhandisi Juma Kijavara amesema ujio wa Meli hiyo ni kutokana na mikakati ya Serikali na mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuhakikisha Bandari hiyo inafanya kazi mda wote mara baada ya kukamilika Kwa maboresho makubwa ambayo yalifanywa na Serikali katika Bandari hiyo.
Akiongea katika hafla ya upokeaji wa Meli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jeneral Marco Gaguti amevionya vyama vya ushirika mkoani Mtwara kuacha mara moja kujihusisha na udanganyifu katika ugawaji wa viutilifu ambavyo vimetolewa na serikali kama ruzuku kwa wakulima wa korosho mkoani hapo.
Gaguti amesema viuatilifu hivyo ambavyo vimetolewa bure na serikali kama ruzuku kwa wakulima wa korosho mkoani Mtwara, na mikoa mingine ya Kusini ni Kwa ajili ya wakulima wa korosho na sio vinginevyo huku akitaka vigawiwe Kwa wahusika pekee bila udanganyifu
“Tuna taarifa kwamba baadhi ya vyma vya ushirika hawagawi hivi viuatilifu ambavyo vinatolewa na serikali kama ilivyokusudiwa na natoa rai kwa wale wanaojihusisha na udanganyifu huo kuacha mara moja,” amesema na kusema serikali itachukua hatua mara moja kwa wale watakoabainika kufanya
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti (aliyevaaa sare ya Jeshi) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (wa tatu kushoto), na Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Alhaji Saad ( wa Kwanza kulia) akiwa katika Bandari akiwa wanashuhudia kuwasili Kwa Meli ya MV YASEMIN ambayo Kwa mara ya kwanza imetia nanga Katika Bandari hiyo mara baada ya kufanyika maboresho makubwa ya kupanua Bandari. Meli za Aina hiyo zilikuwa zinatia nanga Katika Bandari ya Dar Es Salaam na baadae mizigo kusafirishwa kuja Mikoa ya Kusini
No comments: