MABORESHO YALIYOFANYWA KATIKA CHUO CHA UALIMU PATANDI YACHANGIA KUONGEZA KIWANGO CHA TAALUMA

Charles James, Michuzi TV

MABORESHO makubwa yaliyofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika Chuo Cha Ualimu Elimu Maalum Patandi unaelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha taaluma katika Chuo hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo hicho kilichopo Tengeru Mkoani Arusha, Lucian Segesela amesema kuanzia mwaka 2017 hadi sasa Wizara imekua ikikifanya jitahada za kukarabati Chuo hicho kikongwe Nchini ambacho kimekua kikitoa Walimu bora wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Segesela amesema maboresho hayo yamefanyika katika miundombinu ya Mabweni, Madarasa, Maabara na Maktaba, ujenzi wa jengo jipga la utawala pamoja na kupatiwa gari maalum la Afya ambalo ni Land Cruiser mpya.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu imewapatia nakala 270 za vitabu, Kompyuta 30 za kujifunzia na kuendana na teknolojia, projekta ya kufundishia, mashine kubwa ya fotokopi pamoja na kuwapatia mafunzo watumishi wote wa chuo hicho.

" Kwa kweli tunaishukuru sana Serikali yetu imekiona Chuo Cha Patandi kwa kutufanyia maboresho haya ambayo yamesaidia kuongeza kiwango cha taaluma pamoja na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutokana na Serikali kutuongezea pia idadi ya Mabweni," Amesema Mkuu wa Chuo hicho.

Muonekano wa Ujenzi wa Jengo la utawala la Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha ukiendelea ambapo unafanywa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu.
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha wakijifunza kwa TEHAMA ambapo Kompyuta wanazotumia zipatazo 30 zimeletwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ikiwa ni mkakati wa Serikali wa wanafunzi kujifunza kwa TEHAMA.
Muonekano wa baadhi ya Mabweni katika Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha ambao umefanywa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Ujenzi wa jengo la Maabara na Maktaba unaaofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika Chuo Cha Ualimu Elimu Maalum Patandi Mkoani Arusha ukiendelea.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi, Lucia Segesela akisoma taarifa ya maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika chuo hicho.

No comments: