Dovutwa amshauri Waziri Mkuu kassim Majaliwa kuhusu kilimo zao la pamba, utafiti
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANASIASA mkongwe Fahm Dovutwa, ameishauri serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya utafiti wa kufa kwa kilimo cha mazao ambayo yalilimwa kwa wingi katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
Mazao hayo ni minazi, mikorosho, michungwa, miembe ambapo utafiti huo utaisadia serikali kujua utatuzi wa kilimo cha mazao hayo kitaalam.
Dovutwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
“Kutokanan na maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane, watu wa mikoa ya Pwani, tunaomba nafasi zaidi ya ushiriki wa sikukuu hii katika sekta ya kilimo.
“Si kwamba tumefinywa au tumebanwa bali uzalishaji wa mazao ya kilimo mikoa ya Pwani umeshuka,” alisema.
Alisema ajenda hiyo ni ya muda mrefu ili walichelewa kuiwasilisha serikalini ambapo chimbuko la ajenda hiyo ni iliibuliwa mwaka 2014 katika Bunge la Katiba.
“Baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam tulikaa na kutafakari juu ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara tukakubaliana tuiombe serikali mambo mawili,” alieleza Dovutwa.
Jambo la kwanza, miongoni mwa vilimo vikuu katika mikoa ya Pwani ni minazi, miembe, michungwa, korosho imekufa hivyo wanaiomba serikali kupitia Majaliwa ifanye utafiti wa mazao hayo ili kujua utatuzi wake.
Pili, wanaiomba serikali iruhusu mikoa hiyo ilime zao la pamba ambayo inastawi vizuri na kwa ubora kama ile inayolimwa katika mikoa mingine nchini.
“Awali pamba yetu tuliambiwa kuna maaradhi kutoka Msumbiji ambayo inaharibu zao la pamba lakini Msumbiji ambako kulisemwa kuna ugonjwa unaharibu zao la pamba wao wanaendelea kulima hadi leo,” alisema.
Alisema Majaliwa ndiye muhamasishaji mkubwa wa kilimo ndio maana wameona ombi lao lipitie kwani.
Majaliwa amekuwa akihamasisha kilimo kwa wananchi hivyo wanaamini kilimo cha pamba kikiongezewa nguvu katika mikoa hiyo Taifa litapata tija kubwa.
Aliongeza kuwa, miaka ya 1960 kilimo cha pamba kwa mikoa ya Pwani kilisababisha shule zifungwe ili wanafunzi waasidie kuvuna zao hilo mashambani.
Dovutwa alisema anaamini kilimo hicho kikipewa msukumo mzuri mikoa hyo itasonga mbele kwani mwaka 1963 Taifa liliuza nje mazao yenye thamani ya paundi milioni 11, wakati huo bajeti ya nchi ilikuwa milioni 10 ikabaki paundi milioni moja mkononi.
“Tuna mazao mengi ya asili ambayo leo yakipewa nafasi Taifa litasonga mbele kama kilimo kitapewa nafasi yake inayostahili, tatizo la Wamachinga litakuwa historia.
“Huko nyuma kilimo kilipostawi kulikuwa hakuna tatizo la Wamachinga, watu wote walipata maisha katika mikoa yao,” alisisitiza Dovutwa.

No comments: